Nyuma

Hakika muumini hufikia kwa sababu ya tabia zake njema daraja ya mfungaji mwenye kusimama usiku

Kisomo cha Kiarabu Kiarabu Fasaha (MP3)

عن عائشة رضي الله عنها قالت: سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول: «إنَّ المُؤْمِنَ ليُدرِكُ بِحُسْنِ خُلُقِهِ دَرَجَةَ الصَّائِمِ القَائِمِ».

Kutoka kwa Aisha -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Hakika muumini hufikia kwa sababu ya tabia zake njema daraja ya mfungaji mwenye kusimama usiku".

‘Ā’ishah (may Allah be pleased with her) reported: I heard the Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) say: "Verily, a believer can attain, by his good manners, the rank of one who fasts and prays often."

Uislamu umetilia umuhimu mkubwa kurekebisha tabia na ukamilifu wake.

Ubora wa tabia njema, mpaka mja humfikisha daraja ya mfungaji asiyefungua na mwenye kusimama usiku asiyechoka.

Kufunga mchana na kusimama usiku ni amali mbili kubwa, kuna uzito mkubwa sana kwa nafsi, lakini daraja yake ameifikia mwenye tabia njema kwa kupambana na nafsi yake ili kuwa na muamala mzuri na watu.

Rejea na Daraja ya Hadithi

Kitabu na Mlango:
Musnad Ahmad · Hadith Na. HE-5799 (Maadili, Adabu na Tabia Njema · Wema, Uadilifu na Tabia Njema)
Daraja na Mpokezi:
Ni sahihi kwa ushahidi wake mbalimbali · Imepokelewa na Abu Daud na Ahmad
Mfasiri na Chanzo:
HadeethEnc.com — Kiswahili · Chanzo cha Tafsiri ↗
Masharti ya Matumizi:
Leseni ya Maudhui ↗
ahmad:he:5799