Ewe Abuu Dhari utakapopika mchuzi basi zidisha maji yake, na umkumbuke jirani yako
Hukumu za Swala na Tohara
Kiarabu
عَنْ أَبِي ذَرٍّ رَضيَ اللهُ عنهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «يَا أَبَا ذَرٍّ إِذَا طَبَخْتَ مَرَقَةً فَأَكْثِرْ مَاءَهَا، وَتَعَاهَدْ جِيرَانَكَ».
Tafsiri ya Kiswahili
Kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Ewe Abuu Dhari utakapopika mchuzi basi zidisha maji yake, na umkumbuke jirani yako".
English translation
Abu Dharr (may Allah be pleased with him) reported: The Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "O Abu Dharr, if you cook broth, increase its water and take care of your neighbors."
Maelezo
Alimhimiza Mtume rehema na amani ziwe juu yake Abuu Dhari Al-Ghifaari radhi za Allah ziwe juu yake atakapopika mchuzi basi azidishe maji yake na mchuzi wake, na amkumbuke na amtafute jirani yake.
Faida
- Himizo la kuwa na mahusiano mazuri na jirani.
- Sunna ya kupeana zawadi kati ya majirani wawili; kwa sababu hilo linaleta mapenzi na mahaba, na kunakuwa na mkazo zaidi kupeana zawadi huku pindi chakula kinapokuwa na harufu nzuri, na ikajulikana hali ya jirani.
- Himizo la kutenda wema na kila kinachowezekana hata kikiwa kidogo, na kuingiza furaha kwa waislamu.
Jifanyie mazoezi
Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.