Fiqhi, Swala na Ibada
SOMO · Sahih Muslim · Na. HE-5212

Hakuwahi kuswali tena Mtume rehema na amani ziwe juu yake swala yoyote baada kuteremka kwake: "Itakapokuja nusura ya Mwenyezi Mungu na ufunguzi" [An-Naswir:1] Isipokuwa alikuwa akisema ndani yake: "Sub-haanaka Rabbanaa wabihamdika Allaahummagh-firlii, (umetakasika Mola wetu Mlezi na sifa njema ni zako, ewe Mwenyezi Mungu nisamehe)

Hukumu za Swala na Tohara

Kiarabu

عَنْ عَائِشَةَ أُمِّ المُؤْمِنينَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ: مَا صَلَّى النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ صَلاَةً بَعْدَ أَنْ نَزَلَتْ عَلَيْهِ: {إِذَا جَاءَ نَصْرُ اللَّهِ وَالفَتْحُ} [النصر: 1] إِلَّا يَقُولُ فِيهَا: «سُبْحَانَكَ رَبَّنَا وَبِحَمْدِكَ اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي». وعَنْها قَالَتْ: كَانَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يُكْثِرُ أَنْ يَقُولَ فِي رُكُوعِهِ وَسُجُودِهِ: «سُبْحَانَكَ اللهُمَّ رَبَّنَا وَبِحَمْدِكَ، اللهُمَّ اغْفِرْ لِي» يَتَأَوَّلُ الْقُرْآنَ.

Tafsiri ya Kiswahili

Imepokelewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Hakuwahi kuswali tena Mtume rehema na amani ziwe juu yake swala yoyote baada kuteremka kwake: "Itakapokuja nusura ya Mwenyezi Mungu na ufunguzi" [An-Naswir:1] Isipokuwa alikuwa akisema ndani yake: "Sub-haanaka Rabbanaa wabihamdika Allaahummagh-firlii, (umetakasika Mola wetu Mlezi na sifa njema ni zako, ewe Mwenyezi Mungu nisamehe)". Na kutoka kwa Aisha amesema: Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akikithirisha kusema katika rukuu yake na sijida yake: "Sub-haanaka llaahumma Rabbanaa wabihamdika Allaahummagh-firlii" Umetakasika ewe Mwenyezi Mungu, Mola wetu Mlezi, na sifa njema ni zako, ewe Mola wangu Mlezi nisamehe" Akiifasiri Qur'ani.

English translation

‘Ā’ishah, Mother of the Believers, (may Allah be pleased with her) reported: The Prophet (may Allah's peace and blessings be upon him) did not offer a prayer after the revelation of {When there comes Allah’s help and the conquest} [Surat an-Nasr: 1] except that he would say therein: "Subhānaka Rabbana wa bihamdik, Allāhumma ighfir li (Glory and praise be to You, our Lord. O Allah, forgive me)". She also reported: The Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) used to say frequently in his Rukū‘ and Sujūd: "Subhānak Allāhumma Rabbana wa bihamdik, Allāhumma ighfir li (Glory and praise be to You, O Allah, our Lord. O Allah, forgive me)" in compliance with the command in the Qur’an.

Maelezo

Anaeleza mama wa waumini Aisha radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alipoteremshiwa juu yake: "Itakapokuja nusura ya Mwenyezi Mungu na ufunguzi" Akaifasiri Qur'ani na akaanza kuitekeleza amri ya Mwenyezi Mungu Mtukufu katika kauli yake: "Basi zitakase sifa za Mola wako Mlezi na umuombe msamaha", akawa akikithirisha kusema katika rukuu zake na sijida zake wakati wa swala: "Umetakasika" Na ni kukutakasa wewe dhidi ya kila mapungufu yale yasiyokufaa, "Mola wetu Mlezi na sifa njema ni zako" Kwa sifa nzuri kwako kwa ukamilifu wa dhati yako na sifa zako na matendo yako, "Ewe Mwenyezi Mungu nisamehe" na zifute kwangu dhambi zangu, na uziachilie mbali.

Faida

  • Kupendeza kukithirisha dua hii katika rukuu na sijida.
  • Kuomba msamaha mwisho wa umri kuna angalizo la kuhitimisha ibada zote namna hiyo, na hasa hasa swala kwa kuomba msamaha, ili azibe yale yaliyojitokeza ndani yake miongoni mwa mapungufu.
  • Jambo zuri linalotumika kukubaliwa dua kupitia jambo hilo ni kutaja mazuri yake na sifa zake, na kumtakasa dhidi ya mapungufu na aibu.
  • Fadhila ya kuomba msamaha, na kuutafuta katika kila hali.
  • Ukamilifu wa utumwa wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na kutekeleza kwake amri ya Mwenyezi Mungu.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)