Nyuma

Alisema kuniambia mimi Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Soma

Kisomo cha Kiarabu Kiarabu Fasaha (MP3)

عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ مَسْعُودٍ رَضيَ اللهُ عنهُ قَالَ: قَالَ لِي النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «اقْرَأْ عَلَيَّ»، قُلْتُ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، أَأَقْرَأُ عَلَيْكَ، وَعَلَيْكَ أُنْزِلَ؟ قَالَ: «نَعَمْ» فَقَرَأْتُ سُورَةَ النِّسَاءِ حَتَّى أَتَيْتُ إِلَى هَذِهِ الآيَةِ: {فَكَيْفَ إِذَا جِئْنَا مِنْ كُلِّ أُمَّةٍ بِشَهِيدٍ، وَجِئْنَا بِكَ عَلَى هَؤُلاَءِ شَهِيدًا} [النساء: 41]، قَالَ: «حَسْبُكَ الآنَ» فَالْتَفَتُّ إِلَيْهِ، فَإِذَا عَيْنَاهُ تَذْرِفَانِ.

Imepokelewa kutoka kwa Abdullahi bin Masoud -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Alisema kuniambia mimi Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Soma", Nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, Nikusomee vipi, na hali yakuwa Qur'ani iliteremka juu yako? Akasema: "Ndiyo" Nikasoma suratun Nisaai mpaka nikafika katika aya hii: "Basi itakuwaje pindi tukiwaletea kutoka kila Umma shahidi, na tukakuleta wewe kuwa shahidi wa hawa" [An-Nisaai: 41], Akasema: "Inatosha sasa" Nikamgeukia, ghafla nikaona macho yake yakibubujika machozi.

‘Abdullah ibn Mas‘ūd (may Allah be pleased with him) reported: The Prophet (ﷺ) said to me: "Recite to me". I said: O Messenger of Allah, shall I recite to you while it has been revealed to you? He replied: "Yes." So I recited Surat an-Nisā’ until I reached this verse: {How will it be when We bring a witness from every community, and bring you [O Prophet] as a witness against these [people]?} [Surat an-Nisā’: 41] He said: "Enough for now." As I looked at him, I saw that his eyes were shedding tears.

Amesema Nawawi: Sunna ya kusikiliza Qur'ani na kuitegea sikio na kulia wakati ikisomwa, na kuizingatia, na sunna ya kuomba kusomewa na mtu mwingine ili umsikilize, na hii ni njia bora zaidi ya kuielewa na kuizingatia kuliko mtu kusoma mwenyewe.

Kuisikiliza Qur'ani kuna malipo sawa na kuisoma.

Ubora wa Abdallah bin Masoud radhi za Allah ziwe juu yake, kiasi kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alipenda kusikia kutoka katika kinywa chake, na hii inaonyesha pupa ya bin Masoud radhi za Allah ziwe juu yake juu ya kuitafuta Qur'ani na kuihifadhi na kuidhibiti vizuri.

Fadhila ya kulia kwa kumuogopa Mwenyezi Mungu Mtukufu wakati wa kusikia aya zake, ikiwa ni pamoja na kuzingatia kunyamaza, na kimya kizuri, na kutopiga makelele.

Rejea na Daraja ya Hadithi

Kitabu na Mlango:
Sahih al-Bukhari · Hadith Na. 5050 (Qur'ani Tukufu na Fadhila Zake · Usomaji na Kufanyia Kazi Qur'ani)
Daraja na Mpokezi:
Sahihi · Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Mfasiri na Chanzo:
HadeethEnc.com — Kiswahili · Chanzo cha Tafsiri ↗
Masharti ya Matumizi:
Leseni ya Maudhui ↗
bukhari:he:3571