Nyuma

Hakika Mwenyezi Mungu anaridhia kwenu mambo matatu, na anachukia kwenu mambo matatu

Kisomo cha Kiarabu Kiarabu Fasaha (MP3)

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «إِنَّ اللهَ يَرْضَى لَكُمْ ثَلَاثًا، وَيَكْرَهُ لَكُمْ ثَلَاثًا، فَيَرْضَى لَكُمْ: أَنْ تَعْبُدُوهُ، وَلَا تُشْرِكُوا بِهِ شَيْئًا، وَأَنْ تَعْتَصِمُوا بِحَبْلِ اللهِ جَمِيعًا وَلَا تَفَرَّقُوا، وَيَكْرَهُ لَكُمْ: قِيلَ وَقَالَ، وَكَثْرَةَ السُّؤَالِ، وَإِضَاعَةِ الْمَالِ».

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Hakika Mwenyezi Mungu anaridhia kwenu mambo matatu, na anachukia kwenu mambo matatu, basi anaridhia kwenu: Mumuabudu yeye, na wala msimshirikishe na chochote, na mshikamane katika kamba ya Mwenyezi Mungu nyote na wala msifarakane, na anachukia kwenu mambo matatu: Umbeya, na kuuliza uliza sana, na kupoteza mali".

Abu Hurayrah (may Allah be pleased with him) reported: The Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "Verily, Allah is pleased with three things for you and is displeased with three things for you. He is pleased for you: to worship Him, not to associate anything with Him, and to hold fast to the rope of Allah altogether and not to be disunited; and He dislikes for you: idle talk, excessive questioning, and wasting money."

Anapenda Mwenyezi Mungu Mtukufu kutoka kwa waja wake utakasifu katika ibada zake, na anachukia kumkufuru.

Himizo la kushikana katika kamba ya Mwenyezi Mungu Mtukufu; kwakuwa ndani yake kuna umoja na maelewano.

Himizo la umoja, na amri ya kushikamana nao na kuziweka pamoja safu zake, na katazo la kinyume chake kama kufarakana na kuhitilafiana.

Katazo la kukithirisha maneno kwa yale yasiyomuhusu; kwa sababu yakiwa ni ya halali basi ndani yake kuna kupoteza wakati, na yakiwa ya haramu basi kutakuwa na madhambi mengi.

Katazo la kujiingiza katika habari za watu na kufuatilia hali zao na kusimulia kauli zao na matendo yao.

Katazo la kukithirisha maswali katika mambo ya watu.

Uharamu wa kupoteza mali, na himizo la kuzihifadhi na kuzitumia katika yale yanayofaa.

Rejea na Daraja ya Hadithi

Kitabu na Mlango:
Sahih Muslim · Hadith Na. 1715 (Aqidah na Misingi ya Imani · Tawhid na Kumtii Mwenyezi Mungu)
Daraja na Mpokezi:
Sahihi · Imepokelewa Imamu Muslim
Mfasiri na Chanzo:
HadeethEnc.com — Kiswahili · Chanzo cha Tafsiri ↗
Masharti ya Matumizi:
Leseni ya Maudhui ↗
muslim:he:66236