Nyuma

Halitoacha kuendelea kudhihiri kundi katika Umma wangu, mpaka iwajie amri ya Mwenyezi Mungu nao wakiwa katika kudhihiri huko

Kisomo cha Kiarabu Kiarabu Fasaha (MP3)

عَنِ المُغِيرَةِ بْنِ شُعْبَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «لاَ يَزَالُ طَائِفَةٌ مِنْ أُمَّتِي ظَاهِرِينَ، حَتَّى يَأْتِيَهُمْ أَمْرُ اللَّهِ وَهُمْ ظَاهِرُونَ».

Kutoka kwa Mughira bin Shuuba -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Halitoacha kuendelea kudhihiri kundi katika Umma wangu, mpaka iwajie amri ya Mwenyezi Mungu nao wakiwa katika kudhihiri huko".

Al-Mughīrah ibn Shu‘bah (may Allah be pleased with him) reported that the Prophet (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "A group of my Ummah will continue to be victorious until Allah's command comes while they are victorious."

Muujiza wa wazi wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, kwani wasifu huu bado unaendelea Alhamdulillaah, kwanzia zama za Mtume rehema na amani ziwe juu yake mpaka hivi sasa, na bado utaendelea mpaka ije amri ya Mwenyezi Mungu iliyotajwa katika hadithi.

Fadhila za kuwa na msimamo katika haki na kuifanyia kazi, na himizo juu ya hilo.

Kudhihiri kwa dini kuna aina mbili: Ima kudhihiri kwa hoja na ubainifu na uwazi, na ima kudhihiri kwa dola na mhimili, na kudhihiri kulikobakia ni kwa hoja na ubainifu; kwa sababu hoja ya Uislamu ni Qur'ani, nayo iko wazi na inavitawala vitabu vingine visivyokuwa hiyo, lakini aina ya pili ya kudhihiri, ni kudhihiri kwa nguvu ya dola na mhimili, na hii inategemea kulingana na imani na kuwa na nguvu katika ardhi.

Rejea na Daraja ya Hadithi

Kitabu na Mlango:
Sahih Muslim · Hadith Na. HE-65879 (Aqidah na Misingi ya Imani · Tawhid na Kumtii Mwenyezi Mungu)
Daraja na Mpokezi:
Sahihi · Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Mfasiri na Chanzo:
HadeethEnc.com — Kiswahili · Chanzo cha Tafsiri ↗
Masharti ya Matumizi:
Leseni ya Maudhui ↗
muslim:he:65879