Nyuma

Aliniusia mimi kipenzi changu -rehema na amani ziwe juu yake kwa mambo matatu: kufunga siku tatu katika kila mwezi, na rakaa mbili baada ya kuchomoza jua (Dhuhaa), na nisali witiri kabla sijalala

Kisomo cha Kiarabu Kiarabu Fasaha (MP3)

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: أَوْصَانِي خَلِيلِي صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِثَلاَثٍ: صِيَامِ ثَلاَثَةِ أَيَّامٍ مِنْ كُلِّ شَهْرٍ، وَرَكْعَتَيِ الضُّحَى، وَأَنْ أُوتِرَ قَبْلَ أَنْ أَنَامَ.

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: "Aliniusia mimi kipenzi changu -rehema na amani ziwe juu yake kwa mambo matatu: kufunga siku tatu katika kila mwezi, na rakaa mbili baada ya kuchomoza jua (Dhuhaa), na nisali witiri kabla sijalala".

Abu Hurayrah (may Allah be pleased with him) reported: My close friend (may Allah's peace and blessings be upon him) advised me with three: fasting three days of every month, the two Rak‘ahs of Duha, and performing Witr before I sleep."

Kutofautiana kwa usia wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa Masahaba zake: Hii inasababishwa na elimu yake rehema na amani ziwe juu yake ya kujua hali za Masahaba zake, na kile kinachomfaa kila mmoja miongoni mwao, mwenye nguvu kinachomfaa ni Jihadi, na mchamungu kinachomfaa ni ibada, na mwanachuoni kinachomfaa ni elimu, na kuendelea.

Amesema bin Hajari Al-Asqalaani: Katika kauli yake: Kufunga siku tatu katika kila mwezi, kinachoonekana nikuwa makusudio yake ni masiku meupe, ambayo ni: Siku ya tarehe kumi na tatu, kumi na nne, na kumi na tano, katika kalenda ya Hijiria.

Amesema bin Hajari Al-Asqalani: Hapa inaonyesha kuwa inapendeza kuitanguliza witiri kabla ya kulala, na hii kwa mtu ambaye hana uhakika wa kuamka kuswali.

Umuhimu wa matendo haya matatu; kwa sababu ya usia wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwausia idadi kubwa ya Maswahaba zake.

Amesema bin Daqiq Al-Iid katika kauli yake: "Na rakaa mbili za Dhuha": Huenda kataja chache ambazo unapatikana msisitizo wa kuzifanya, na katika hili kuna dalili ya kuwa Dhuha ni sunna, nakuwa kwa uchache ni rakaa mbili.

Wakati wa swala ya Dhuha: Ni baada ya kuchomoza Jua kwa robo saa takriban, na unakwenda wakati wake mpaka kabla ya Adhuhuri kwa dakika kumi takriban, na idadi: Kwa uchache ni rakaa mbili, na zimetofautiana kauli za wanachuoni kuhusu wingi wake; wakasema: Rakaa nane, na wakasema: Hakuna kiwango cha wingi wake.

Wakati wa witiri: Baada ya swala ya Ishaa mpaka kuchomoza Alfajiri, na uchache wake ni rakaa moja, na wingi wake ni rakaa kumi na moja.

Rejea na Daraja ya Hadithi

Kitabu na Mlango:
Sahih Muslim · Hadith Na. 721 (Fiqhi, Swala na Ibada · Hukumu za Swala na Tohara)
Daraja na Mpokezi:
Sahihi · Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Mfasiri na Chanzo:
HadeethEnc.com — Kiswahili · Chanzo cha Tafsiri ↗
Masharti ya Matumizi:
Leseni ya Maudhui ↗
muslim:he:4538