Nyuma

Nipeni ahadi ya utiifu ya kuwa msimshirikishe Mwenyezi Mungu na kitu chochote, na wala msiibe, na wala msizini

Kisomo cha Kiarabu Kiarabu Fasaha (MP3)

عَنْ عُبَادَةَ بْنِ الصَّامِتِ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ، وَكَانَ شَهِدَ بَدْرًا، وَهُوَ أَحَدُ النُّقَبَاءِ لَيْلَةَ العَقَبَةِ: أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ، وَحَوْلَهُ عِصَابَةٌ مِنْ أَصْحَابِهِ: «بَايِعُونِي عَلَى أَلَّا تُشْرِكُوا بِاللَّهِ شَيْئًا، وَلاَ تَسْرِقُوا، وَلاَ تَزْنُوا، وَلاَ تَقْتُلُوا أَوْلاَدَكُمْ، وَلاَ تَأْتُوا بِبُهْتَانٍ تَفْتَرُونَهُ بَيْنَ أَيْدِيكُمْ وَأَرْجُلِكُمْ، وَلاَ تَعْصُوا فِي مَعْرُوفٍ، فَمَنْ وَفَى مِنْكُمْ فَأَجْرُهُ عَلَى اللَّهِ، وَمَنْ أَصَابَ مِنْ ذَلِكَ شَيْئًا فَعُوقِبَ فِي الدُّنْيَا فَهُوَ كَفَّارَةٌ لَهُ، وَمَنْ أَصَابَ مِنْ ذَلِكَ شَيْئًا ثُمَّ سَتَرَهُ اللَّهُ فَهُوَ إِلَى اللَّهِ، إِنْ شَاءَ عَفَا عَنْهُ وَإِنْ شَاءَ عَاقَبَهُ» فَبَايَعْنَاهُ عَلَى ذَلِكَ.

Kutoka kwa Ubada bin Swamiti radhi za Allah ziwe juu yake, na alikuwa miongoni mwa walioshuhudia vita vya Badri, naye alikuwa ni mmoja wa vigogo katika usiku wa Aqaba: Ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alisema na pembezoni mwake kukiwa na jopo la Maswahaba zake: "Nipeni ahadi ya utiifu ya kuwa msimshirikishe Mwenyezi Mungu na kitu chochote, na wala msiibe, na wala msizini, na wala msiwauwe watoto wenu, na wala msilete uzushi mtakouzua kwa mikono yenu na miguu yenu, na wala msiasi katika wema, basi atakayeyatimiza hayo miongoni mwenu basi malipo yake yatakuwa juu ya Mwenyezi Mungu, na atakayetenda lolote katika hayo akaadhibiwa katika dunia basi hiyo ndiyo kafara kwake, na atakayetenda lolote katika hayo kisha Mwenyezi Mungu akamsitiri basi hilo litabakia kwa Mwenyezi Mungu akitaka atamsamehe na akitaka atamuadhibu" Tukampa ahadi ya utiifu juu ya hayo.

‘Ubādah ibn as-Sāmit (may Allah be pleased with him), who witnessed Badr and was one of the chiefs chosen to represent his tribe on the night of ‘Aqabah, reported: The Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said, and around him was a group of his Companions: "Give me your pledge that you will not associate anything with Allah, that you will not steal, that you will not commit adultery, that you will not kill your children, that you will not bring forth slander you have invented between your hands and legs, and that you will not disobey in righteousness. Whoever among you fulfills these, his reward is with Allah. And whoever commits any of these and is punished in this world, it will be an expiation for him. And whoever commits any of these and Allah covers him, then it is up to Allah; if He wills, He will pardon him, and if He wills, He will punish him." So we gave him our pledge on that.

Kumebainishwa mambo yaliyoambatana na ahadi ya Aqaba ya kwanza huko Makka kabla hawajafaradhishiwa Jihadi.

Amesema As-Sanadi: Kauli yake: "Katika wema": Haifichikani kuwa amri zake zote ni wema na haifikiriki kuwa na kinyume chake, kauli yake: "katika wema" hii ilikuwa ni kwa ajili ya kutanabahisha sababu ya kutii na kwamba hakuna kumtii kiumbe katika jambo lisilokuwa jema, na kwamba ni sharti katika utii kuwe na wema katika ahadi, na si utii wa moja kwa moja.

Amesema Muhammadi bin Suleiman Attaimi na wengineo: Ametaja swala la mauaji ya watoto pekee; kwa sababu ni mauaji na ni kukata ukoo, hivyo kutilia umuhimu katazo hilo kunakuwa na mkazo zaidi, na ni kwa sababu hilo lilikuwa limezagaa sana kwao, jambalo ni kuwazika watoto wa kike na kuwauwa watoto wa kiume kwa kuhofia umasikini, au kawataja maalumu; ili wasijitetee kwa hilo.

Amesema Nawawi: Ujumla wa hadithi hii umeondolewa kwa kauli yake Mtukufu: "Hakika Mwenyezi Mungu hasamehi kushirikishwa", Mwenye kuritadi anapouawa kwa sababu ya kutoka katika dini kuuawa hakuwi kafara kwake.

Amesema Al-Kadhi Iyadhi: Wamesema wanachuoni wengi kuwa adhabu za kisheria ni kafara.

Rejea na Daraja ya Hadithi

Kitabu na Mlango:
Sahih al-Bukhari · Hadith Na. 18 (Maadili, Adabu na Tabia Njema · Wema, Uadilifu na Tabia Njema)
Daraja na Mpokezi:
Sahihi · Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Mfasiri na Chanzo:
HadeethEnc.com — Kiswahili · Chanzo cha Tafsiri ↗
Masharti ya Matumizi:
Leseni ya Maudhui ↗
bukhari:he:66210