Nyuma

Moyo wa mzee huendelea kuwa kijana katika mambo mawili: Katika kupenda dunia na matumaini ya muda mrefu

Kisomo cha Kiarabu Kiarabu Fasaha (MP3)

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: «لاَ يَزَالُ قَلْبُ الكَبِيرِ شَابًّا فِي اثْنَتَيْنِ: فِي حُبِّ الدُّنْيَا وَطُولِ الأَمَلِ».

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Moyo wa mzee huendelea kuwa kijana katika mambo mawili: Katika kupenda dunia na matumaini ya muda mrefu".

Abu Hurayrah (may Allah be pleased with him) reported: I heard the Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) say: "The heart of an elderly person remains young in two things: in the love of this world and long hopes."

Kumebainishwa tabia alioumbwa nayo mwanadamu, nayo ni kuipenda dunia na matumaini marefu.

Hapa kuna ishara ya kuonyesha ubaya wa kuwa na matumaini ya muda mrefu, na pupa ya kukusanya mali, na hilo linachochea kujiandaa na kifo na ubora wa kutoa sadaka kwa mwenye uwezo, na masikini kujizuia kuomba.

Mambo yanayopendeka zaidi kwa mwanadamu ni nafsi yake, kwani anatamani iendelee kubakia, akapenda kwa hilo kuwa na umri mrefu, na akapenda mali; kwa sababu ni katika sababu kubwa za kudumu kwa afya na starehe, kila anapohisi kukaribia kumalizika kwa hilo basi mapenzi yanazidi kuwa makubwa, na hamu yake ya kutamani idumu inaongezeka.

Rejea na Daraja ya Hadithi

Kitabu na Mlango:
Sahih al-Bukhari · Hadith Na. 6420 (Maadili, Adabu na Tabia Njema · Wema, Uadilifu na Tabia Njema)
Daraja na Mpokezi:
Sahihi · Imepokelewa na Al-Bukhaariy
Mfasiri na Chanzo:
HadeethEnc.com — Kiswahili · Chanzo cha Tafsiri ↗
Masharti ya Matumizi:
Leseni ya Maudhui ↗
bukhari:he:66221