Nyuma

Atakayesema nimeridhia Mwenyezi Mungu kuwa Mola, na kuwa Uislamu ni dini, na Muhammadi kuwa Mtume, basi atastahiki kwake Papo

Kisomo cha Kiarabu Kiarabu Fasaha (MP3)

عَن أَبي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «مَنْ قَالَ: رَضِيتُ بِاللَّهِ رَبًّا، وَبِالْإِسْلَامِ دِينًا، وَبِمُحَمَّدٍ رَسُولًا، وَجَبَتْ لَهُ الْجَنَّةُ».

Kutoka kwa Abuu Saidi Al-Khudri radhi za Allah ziwe juu yake, yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Atakayesema nimeridhia Mwenyezi Mungu kuwa Mola, na kuwa Uislamu ni dini, na Muhammadi kuwa Mtume, basi atastahiki kwake Papo".

Abu Sa‘īd al-Khudri (may Allah be pleased with him) reported that the Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "Whoever says: Radītu billāhi rabban, wa bil-Islāmi dīnan, wa bi Muhammadin rasūla (I am pleased with Allah as a Lord, with Islam as a religion, with Muhammad as a Messenger), Paradise is guaranteed for him."

Himizo la kusema dua hii, na kumebainishwa thawabu zinazoambatana nayo.

Kumridhia Mwenyezi Mungu kuwa Mola, kunaambatana na mtu kutomuabudu asiyekuwa yeye Mtukufu.

Kumridhia Muhammadi rehema na amani ziwe juu yake kuwa Nabii na Mtume, kunaambatana na kumtii rehema na amani ziwe juu yake na kutii sunna zake.

Kuridhia Uislamu kuwa dini ni kuridhia yale aliyoyachagua Mwenyezi Mungu kwa waja wake.

Sunna ya kusema dua hii wakati wa shahada mbili baada kusikia Adhana, kama ilivyokuja katika riwaya zingine.

Na imekuja katika hadithi nyingine sunna ya kuomba dua hii wakati wa asubuhi na jioni.

Rejea na Daraja ya Hadithi

Kitabu na Mlango:
Sunan Abu Dawud · Hadith Na. 1529 (Maadili, Adabu na Tabia Njema · Wema, Uadilifu na Tabia Njema)
Daraja na Mpokezi:
Sahihi · Imepokelewa na Abu Daud
Mfasiri na Chanzo:
HadeethEnc.com — Kiswahili · Chanzo cha Tafsiri ↗
Masharti ya Matumizi:
Leseni ya Maudhui ↗
abudawud:he:65906