Nyuma

Asiangalie mwanaume katika uchi wa mwanaume mwenzie, wala mwanamke kutazama uchi wa mwanamke mwenzie

Kisomo cha Kiarabu Kiarabu Fasaha (MP3)

عَن أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ رضي الله عنه أَنَّ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «لَا يَنْظُرُ الرَّجُلُ إِلَى عَوْرَةِ الرَّجُلِ، وَلَا الْمَرْأَةُ إِلَى عَوْرَةِ الْمَرْأَةِ، وَلَا يُفْضِي الرَّجُلُ إِلَى الرَّجُلِ فِي ثَوْبٍ وَاحِدٍ، وَلَا تُفْضِي الْمَرْأَةُ إِلَى الْمَرْأَةِ فِي الثَّوْبِ الْوَاحِدِ».

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Saidi Al-Khudri -Radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Asiangalie mwanaume katika uchi wa mwanaume mwenzie, wala mwanamke kutazama uchi wa mwanamke mwenzie, na wala asijifunike mwanaume na mwanaume mwenzie shuka moja, na wala mwanamke asijifunike na mwanamke mwenzie shuka moja".

Abu Sa‘īd al-Khudri (may Allah be pleased with him) reported that the Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "A man must not look at another man's ‘Awrah (must-cover body part), nor must a woman look at another woman's ‘Awrah; neither should two men lie undressed under one attire, nor should two women lie undressed under one attire."

Katazo la kutazama uchi, isipokuwa mume na mke wake.

Hima ya Uislamu juu kuisafisha jamii, na kufunga njia zinazopelekea katika machafu.

Inaruhusiwa kuangalia uchi kukiwa na haja ya kufanya hivyo, kama matibabu na mfano wake, na isiwe kwa matamanio.

Muislamu ameamrishwa kusitiri uchi wake na kuinamisha macho yake kutotazama uchi wa mwenzie.

Kumetajwa pekee wanaume kuwatazama wanaume wenzao na wanawake kuwatazama wanawake wenzao; kwa sababu ndio kishawishi kikubwa katika kutazama na kufunua uchi.

Rejea na Daraja ya Hadithi

Kitabu na Mlango:
Sahih Muslim · Hadith Na. 338 (Maadili, Adabu na Tabia Njema · Wema, Uadilifu na Tabia Njema)
Daraja na Mpokezi:
Sahihi · Imepokelewa Imamu Muslim
Mfasiri na Chanzo:
HadeethEnc.com — Kiswahili · Chanzo cha Tafsiri ↗
Masharti ya Matumizi:
Leseni ya Maudhui ↗
muslim:he:8904