Nyuma

Rudi kaswali, kwani wewe hujaswali

Kisomo cha Kiarabu Kiarabu Fasaha (MP3)

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه: أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ دَخَلَ المَسْجِدَ فَدَخَلَ رَجُلٌ، فَصَلَّى، فَسَلَّمَ عَلَى النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَرَدَّ وَقَالَ: «ارْجِعْ فَصَلِّ، فَإِنَّكَ لَمْ تُصَلِّ»، فَرَجَعَ يُصَلِّي كَمَا صَلَّى، ثُمَّ جَاءَ، فَسَلَّمَ عَلَى النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَ: «ارْجِعْ فَصَلِّ، فَإِنَّكَ لَمْ تُصَلِّ» ثَلاَثًا، فَقَالَ: وَالَّذِي بَعَثَكَ بِالحَقِّ مَا أُحْسِنُ غَيْرَهُ، فَعَلِّمْنِي، فَقَالَ: «إِذَا قُمْتَ إِلَى الصَّلاَةِ فَكَبِّرْ، ثُمَّ اقْرَأْ مَا تَيَسَّرَ مَعَكَ مِنَ القُرْآنِ، ثُمَّ ارْكَعْ حَتَّى تَطْمَئِنَّ رَاكِعًا، ثُمَّ ارْفَعْ حَتَّى تَعْدِلَ قَائِمًا، ثُمَّ اسْجُدْ حَتَّى تَطْمَئِنَّ سَاجِدًا، ثُمَّ ارْفَعْ حَتَّى تَطْمَئِنَّ جَالِسًا، وَافْعَلْ ذَلِكَ فِي صَلاَتِكَ كُلِّهَا».

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliingia msikitini kisha akaingia mtu mmoja, akaswali, kisha akamsalimia Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akajibu salamu, na akasema: "Rudi kaswali, kwani wewe hujaswali", akarudia kuswali kama alivyoswali mwanzo, kisha akaja, akamsalimia Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasema: "Rudi kaswali kwani wewe hujaswali" (akafanya hivyo) Mara tatu, akasema: "Namuapa yule aliyekutuma kwa haki, siwezi kuswali vizuri zaidi ya hivyo, basi naomba nifundishe, akasema: "Utakaposimama katika swala basi toa takbira (sema: Allaahu Akbaru), kisha soma kiasi chepesi ulichonacho katika Qur'ani, kisha rukuu mpaka utulizane ukiwa umerukuu, kisha nyanyuka mpaka ulingane wima, kisha sujudu mpaka utulizane ukiwa umesujudu, kisha nyanyuka mpaka utulizane ukiwa umekaa, na ufanye hivyo katika swala yako yote".

Abu Hurayrah (may Allah be pleased with him) reported: The Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) entered the mosque, and then a man came in and prayed. He greeted the Prophet (may Allah's peace and blessings be upon him), who responded and said: "Go back and pray, for you have not prayed." He went back and prayed as he had prayed, then, he came to the Prophet (may Allah's peace and blessings be upon him) and greeted him. He said: "Go back and pray, for you have not prayed," three times. So, he said: By the One Who sent you with the truth, I cannot do better than that. So teach me. He said: "When you stand to pray, say Takbīr (Allāhu Akbar), then recite whatever you can of the Qur’an; then bow until you are at ease in bowing; then rise until you are standing up straight; then prostrate until you are at ease in prostration; and then sit up until you are at ease in sitting. Do that throughout your prayer."

Nguzo hizi za swala hazidondoki kwa kusahau wala kwa ujinga, kwa dalili ya kuamrishwa mwenye kuswali kurudia, na wala hakutosheka Mtume rehema na amani ziwe juu yake na kumfundisha pekee.

Kutulia ni nguzo miongoni mwa nguzo za swala.

Amesema Nawawi: Na hapa nikuwa atakayepunguza baadhi ya wajibu za swala basi haitoswihi swala yake.

Amesema Nawawi: Na ndani ya hili kuna kumhurumia mwenye kujifunza na mjinga na kuwa mpole kwake, na kumuwekea wazi maswala na kufupisha makusudio, na kufupisha katika haki zake yale ya muhimu pasina yale yenye kukamilisha, ambayo yanategemea mpaka kuyahifadhi na kuyatekeleza.

Amesema Nawawi: Na hapa nikuwa Mufti akiulizwa kuhusu jambo na kukawa na jambo jingine muhimu zaidi analolihitajia muulizaji lakini hakuliulizia basi ni sunna alieleze, na hii inakuwa ni katika nasaha na si katika kuzungumza yasiyomuhusu.

Fadhila za kukiri mapungufu, kwa kauli yake: "Siwezi kufanya vizuri zaidi ya hivyo, basi nifundishe".

Amesema bin Hajari: Hapa kuna kuamrisha mema na kukataza maovu, na mwenye kujifunza kumuomba mwalimu amfundishe.

Sunna ya kutoa salamu wakati wa kukutana, na uwajibu wa kuitikia, na kwamba inapendeza kukutana mara kwa mara hata kama muda utakaribiana, na kwamba ni lazima kuitikia kwa kila mara.

Rejea na Daraja ya Hadithi

Kitabu na Mlango:
Sahih Muslim · Hadith Na. HE-3185 (Muslim — bado haijapangwa (ya muda) · Hadith zilizogunduliwa hivi karibuni (ya muda))
Daraja na Mpokezi:
Sahihi · Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Mfasiri na Chanzo:
HadeethEnc.com — Kiswahili (jina la mtafsiri halijatajwa katika API) · Chanzo cha Tafsiri ↗
Masharti ya Matumizi:
Leseni ya Maudhui ↗
muslim:hadeethenc-provisional:3185