عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «قَالَ اللَّهُ تَبَارَكَ وَتَعَالَى: أَعْدَدْتُ لِعِبَادِي الصَّالِحِينَ، مَا لاَ عَيْنٌ رَأَتْ، وَلاَ أُذُنٌ سَمِعَتْ، وَلاَ خَطَرَ عَلَى قَلْبِ بَشَرٍ» قَالَ أَبُو هُرَيْرَةَ: اقْرَؤُوا إِنْ شِئْتُمْ: {فَلاَ تَعْلَمُ نَفْسٌ مَا أُخْفِيَ لَهُمْ مِنْ قُرَّةِ أَعْيُنٍ} [السجدة: 17].
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Amesema Allah Aliyetakasika na kutukuka: Nimewaandalia waja wangu wema, vitu ambavyo jicho halijawahi kuona, wala sikio kusikia, wala haijawahi kupita katika fikira ya moyo wa binadamu yeyote" Akasema Abuu Huraira: Someni mkitaka: "Basi nafsi yoyote haijui yale waliyofichiwa miongoni mwa mambo yenye kutuliza macho" [As-Sajida: 17).
Abu Hurayrah (may Allah be pleased with him) reported that the Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "Allah, the Blessed and Exalted, said: I have prepared for My righteous slaves what no eye has ever seen, no ear has ever heard, and no human heart has ever imagined," Abu Hurayrah said: Recite, if you wish: {No soul knows what delights are kept hidden for them.} [Surat as-Sajdah: 17]
Hadithi hii ni katika zile anazozipokea Mtume rehema na amani ziwe juu yake kutoka kwa Mola wake Mlezi, na huitwa Hadithil Qudsi au Hadithil Ilahi, nayo ni ile ambayo tamko lake na maana yake inatoka kwa Allah, isipokuwa haina upekee kama wa Qur'ani inaojipambanua nayo kwa vingine, kama kisomo chake kutumika katika ibada, na kuwa twahara kabla ya kusoma, na kuwashinda watu kwa changamoto zake, na mengineyo.
Himizo la kufanya matendo ya utiifu na kuacha maovu; ili kufaulu kwa kuyapata yale aliyoyaandaa Mwenyezi Mungu kwa waja wake wema.
Mwenyezi Mungu hakutuonyesha ndani ya kitabu chake wala mafundisho ya Mtume wake yote yaliyoko peponi, na kwamba ambayo hatujayafahamu ni makubwa kuliko tuliyoyafahamu.
Kumebainishwa ukamilifu wa neema za peponi, na kwamba wakazi wake watapata katika mambo ya kufurahisha yasiyokuwa na tabu wala mawazo ya namna kupatikana kwake.
Starehe za dunia ni zenye kuisha na Akhera ndio bora na yenye kubakia.