Nyuma

Aina mbili za watu ni miongoni mwa watu wa motoni, sijawaona (katika zama zake Mtume), watu walio na mijeledi mithili ya mikia ya Ng'ombe wakiwapiga watu, na wanawake waliovaa na wako uchi, wanenguaji wakatikaji

Kisomo cha Kiarabu Kiarabu Fasaha (MP3)

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «صِنْفَانِ مِنْ أَهْلِ النَّارِ لَمْ أَرَهُمَا، قَوْمٌ مَعَهُمْ سِيَاطٌ كَأَذْنَابِ الْبَقَرِ يَضْرِبُونَ بِهَا النَّاسَ، وَنِسَاءٌ كَاسِيَاتٌ عَارِيَاتٌ مُمِيلَاتٌ مَائِلَاتٌ، رُؤُوسُهُنَّ كَأَسْنِمَةِ الْبُخْتِ الْمَائِلَةِ، لَا يَدْخُلْنَ الْجَنَّةَ، وَلَا يَجِدْنَ رِيحَهَا، وَإِنَّ رِيحَهَا لَيُوجَدُ مِنْ مَسِيرَةِ كَذَا وَكَذَا».

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Aina mbili za watu ni miongoni mwa watu wa motoni, sijawaona (katika zama zake Mtume), watu walio na mijeledi mithili ya mikia ya Ng'ombe wakiwapiga watu, na wanawake waliovaa na wako uchi, wanenguaji wakatikaji, vichwa vyao ni kama nundu za Ngamia zenye kuyumba (huku na kule), hawa, hawatoingia peponi, na wala hawatoipata harufu yake, na hakika harufu yake hupatikana umbali wa masafa kadhaa wa kadhaa".

Abu Hurayrah (may Allah be pleased with him) reported that the Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "There are two types of the dwellers of Hellfire whom I have not seen: people with whips like the tails of cows with which they beat people, and women who will be dressed yet naked, inviting to evil, and they themselves are inclined to it. Their heads will appear like the humps of the Bactrian camels, inclined to one side. They will not enter Paradise nor will they smell its fragrance; the fragrance that is smelled from such-and-such a distance."

Uharamu wa kuwapiga watu na kuwaudhi bila dhambi yoyote waliyoifanya au dhambi walilolichuma.

Ni haramu kuwasaidia watenda dhulma katika dhulma yao.

Ni haramu wanawake kutoka bila haja ya msingi na kujiachia katika mavazi, na kuvaa nguo za kubana zenye kuonyesha, zinazoonyesha uchi au kuuchora.

Kumhimiza mwanamke wa kiislamu juu ya kushikamana na amri za Mwenyezi Mungu, na kujiweka mbali na yale yenye kumkasirisha, na kumfanya astahiki kupata adhabu chungu na ya kudumu Akhera.

Hadithi hii ni dalili ya utume wake rehema na amani ziwe juu yake, kiasi kwamba ametoa habari rehema na amani ziwe juu yake kuhusu mambo ya ghaibu ambayo hayajatokea, na yametokea kama alivyoeleza.

Rejea na Daraja ya Hadithi

Kitabu na Mlango:
Sahih Muslim · Hadith Na. 2128 (Maadili, Adabu na Tabia Njema · Wema, Uadilifu na Tabia Njema)
Daraja na Mpokezi:
Sahihi · Imepokelewa Imamu Muslim
Mfasiri na Chanzo:
HadeethEnc.com — Kiswahili · Chanzo cha Tafsiri ↗
Masharti ya Matumizi:
Leseni ya Maudhui ↗
muslim:he:8903