Nyuma

Imani ni zaidi ya vitengo sabini au zaidi ya sitini, bora yake ni kauli ya Laa ilaaha illa llaah, na ya chini yake ni kuondoa udhia barabarani

Kisomo cha Kiarabu Kiarabu Fasaha (MP3)

عن أبي هريرة رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: «الْإِيمَانُ بِضْعٌ وَسَبْعُونَ -أَوْ بِضْعٌ وَسِتُّونَ- شُعْبَةً، فَأَفْضَلُهَا قَوْلُ لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ، وَأَدْنَاهَا إِمَاطَةُ الْأَذَى عَنِ الطَّرِيقِ، وَالْحَيَاءُ شُعْبَةٌ مِنَ الْإِيمَانِ».

Imepolelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema: Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Imani ni zaidi ya vitengo sabini au zaidi ya sitini, bora yake ni kauli ya Laa ilaaha illa llaah, na ya chini yake ni kuondoa udhia barabarani, na haya ni sehemu katika imani".

Abu Hurayrah (may Allah be pleased with him) reported: The Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "Faith has over seventy branches - or over sixty branches - the most excellent of which is the declaration that 'lā ilāha illa Allah (there is no god but Allah)', and the lowest of which is the removal of what is harmful from the way; and modesty is a branch of faith."

Imani inadaraja baadhi yake ni bora kuliko zingine.

Imani ni kauli na matendo na itikadi.

Kumuonea haya Allah Mtukufu hupelekea: Kuwa asikuone pale alipokukataza, na asikukose pale alipokuamrisha.

Kutajwa idadi hakumaanishi kuishia hapo, bali inamaanisha wingi wa matendo ya imani, kwani waarabu wanaweza kutaja idadi ya kitu na wasimaanishe kukanusha idadi nyingine isiyokuwa hiyo.

Rejea na Daraja ya Hadithi

Kitabu na Mlango:
Sahih Muslim · Hadith Na. 35 (Aqidah na Misingi ya Imani · Tawhid na Kumtii Mwenyezi Mungu)
Daraja na Mpokezi:
Sahihi · Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Mfasiri na Chanzo:
HadeethEnc.com — Kiswahili · Chanzo cha Tafsiri ↗
Masharti ya Matumizi:
Leseni ya Maudhui ↗
muslim:he:6468