Utafiti na Ramani ya Maarifa
UTAFITI

Linganisha Hadith

Ufanano wa maneno: 29%

Ufanano huu unategemea maneno yanayoshirikiana tu. Si hukumu ya kielimu kuhusu maana au daraja la hadith.

Maneno yanayoshirikiana

hurairashetaniradhi

Sahih al-Bukhari · Na. HE-4192

Wema, Uadilifu na Tabia Njema

عن أبي هريرة رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : «من رآني في المنام فَسَيَرَانِي في اليَقظة -أو كأنما رآني في الْيَقَظَةِ- لا يَتَمَثَّلُ الشيطان بي».

Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake-: "Atakayeniona mimi ndotoni basi ataniona akiwa macho -au ni kana kwamba kaniona akiwa macho- hajifananishi shetani na mimi".

Daraja: Sahihi

Sahih al-Bukhari · Na. HE-8377

Hukumu za Swala na Tohara

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «إِذَا اسْتَيْقَظَ أَحَدُكُمْ مِنْ مَنَامِهِ فَلْيَسْتَنْثِرْ ثَلَاثَ مَرَّاتٍ، فَإِنَّ الشَّيْطَانَ يَبِيتُ عَلَى خَيَاشِيمِهِ».

Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake: Kuwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakapoamka mmoja wenu kutoka usingizini mwake basi na apenge kwa maji mara tatu, kwani Shetani hulala ndani ya tundu zake za pua".

Daraja: Sahihi