Hadithi 40 za An-Nawawi · Na. 37
Uadilifu na Neema za Allah Katika Kulipa Mema na Maovu
عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فِيمَا يَرْوِيهِ عَنْ رَبِّهِ تَبَارَكَ وَتَعَالَى قَالَ: «إِنَّ اللَّهَ كَتَبَ الْحَسَنَاتِ وَالسَّيِّئَاتِ ثُمَّ بَيَّنَ ذَلِكَ: فَمَنْ هَمَّ بِحَسَنَةٍ فَلَمْ يَعْمَلْهَا كَتَبَهَا اللَّهُ عِنْدَهُ حَسَنَةً كَامِلَةً، وَإِنْ هَمَّ بِهَا فَعَمِلَهَا كَتَبَهَا اللَّهُ عِنْدَهُ عَشْرَ حَسَنَاتٍ إِلَى سَبْعِمِائَةِ ضِعْفٍ إِلَى أَضْعَافٍ كَثِيرَةٍ، وَإِنْ هَمَّ بِسَيِّئَةٍ فَلَمْ يَعْمَلْهَا كَتَبَهَا اللَّهُ عِنْدَهُ حَسَنَةً كَامِلَةً، وَإِنْ هَمَّ بِهَا فَعَمِلَهَا كَتَبَهَا اللَّهُ سَيِّئَةً وَاحِدَةً».
Kutoka kwa Ibn Abbas (Radhi za Allah ziwe juu yao) kutoka kwa Mjumbe wa Allah katika yale anayoyapokea kutoka kwa Mola wake Mlezi Aliyetukuka kuwa amesema: "Hakika Allah amekwisha andika mambo mema na maovu kisha akafafanua hilo: Mwenye kudhamiria kutenda tendo jema kisha asilitende, Allah Humwandikia kwake tendo jema kamili. Na akidhamiria kisha akalitenda, Allah Humwandikia mema kumi hadi mara mia saba na kuzidi maradufu mengi. Na akidhamiria tendo ovu kisha asilitende, Allah Humwandikia kwake tendo jema kamili, na akidhamiria kisha akalitenda, Allah Humwandikia kosa moja tu."
Daraja: Sahihi