Utafiti na Ramani ya Maarifa
UTAFITI

Linganisha Hadith

Ufanano wa maneno: 12%

Ufanano huu unategemea maneno yanayoshirikiana tu. Si hukumu ya kielimu kuhusu maana au daraja la hadith.

Maneno yanayoshirikiana

kumshirikishachochotepeponiradhijambo

Hadithi 40 za An-Nawawi · Na. 29

Milango ya Kheri na Mhimili Mkuu wa Dini

عَنْ مُعَاذِ بْنِ جَبَلٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: قُلْتُ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، أَخْبِرْنِي بِعَمَلٍ يُدْخِلُنِي الْجَنَّةَ وَيُبَاعِدُنِي عَنِ النَّارِ، قَالَ: «لَقَدْ سَأَلْتَ عَنْ عَظِيمٍ، وَإِنَّهُ لَيَسِيرٌ عَلَى مَنْ يَسَّرَهُ اللَّهُ عَلَيْهِ: تَعْبُدُ اللَّهَ لاَ تُشْرِكُ بِهِ شَيْئاً، وَتُقِيمُ الصَّلاَةَ، وَتُؤْتِيَ الزَّكَاةَ، وَتَصُومُ رَمَضَانَ، وَتَحُجَّ الْبَيْتَ»... ثُمَّ قَالَ: «أَلاَ أُخْبِرُكَ بِمَلاَكِ ذَلِكَ كُلِّهِ؟» قُلْتُ: بَلَى يَا نَبِيَّ اللَّهِ. فَأَخَذَ بِلِسَانِهِ وَقَالَ: «كُفَّ عَلَيْكَ هَذَا».

Kutoka kwa Mu'adh bin Jabal (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesema: Nilisema: Ewe Mjumbe wa Allah! Nieleze amali itakayoniingiza Peponi na kunitenga mbali na Moto. Akasema: "Hakika umeuliza jambo kubwa, nalo ni jepesi kwa yule ambaye Allah Amemfanyia wepesi: Muabudu Allah bila kumshirikisha na chochote, simamisha Swala, toa Zaka, funga Ramadhani, na uhiji Nyumba Tukufu... Kisha akasema: Je, nisikujulishe nguzo inayomiliki na kulinda haya yote? Nikasema: Ndio ewe Nabii wa Allah. Akakamata ulimi wake akasema: Uzuie huu usiseme hovyo!"

Daraja: Sahihi

Musnad Ahmad · Na. HE-65014

Wema, Uadilifu na Tabia Njema

عَنْ خُرَيْمِ بْنِ فَاتِكٍ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «الْأَعْمَالُ سِتَّةٌ، وَالنَّاسُ أَرْبَعَةٌ، فَمُوجِبَتَانِ، وَمِثْلٌ بِمِثْلٍ، وَحَسَنَةٌ بِعَشْرِ أَمْثَالِهَا، وَحَسَنَةٌ بِسَبْعِ مِائَةٍ، فَأَمَّا الْمُوجِبَتَانِ: فَمَنْ مَاتَ لَا يُشْرِكُ بِاللهِ شَيْئًا دَخَلَ الْجَنَّةَ، وَمَنْ مَاتَ يُشْرِكُ بِاللهِ شَيْئًا دَخَلَ النَّارَ، وَأَمَّا مِثْلٌ بِمِثْلٍ: فَمَنْ هَمَّ بِحَسَنَةٍ حَتَّى يَشْعُرَهَا قَلْبُهُ، وَيَعْلَمَهَا اللهُ مِنْهُ كُتِبَتْ لَهُ حَسَنَةً، وَمَنْ عَمِلَ سَيِّئَةً، كُتِبَتْ عَلَيْهِ سَيِّئَةً، وَمَنْ عَمِلَ حَسَنَةً فَبِعَشْرِ أَمْثَالِهَا، وَمَنْ أَنْفَقَ نَفَقَةً فِي سَبِيلِ اللهِ فَحَسَنَةٌ بِسَبْعِ مِائَةٍ، وَأَمَّا النَّاسُ، فَمُوَسَّعٌ عَلَيْهِ فِي الدُّنْيَا مَقْتُورٌ عَلَيْهِ فِي الْآخِرَةِ، وَمَقْتُورٌ عَلَيْهِ فِي الدُّنْيَا مُوَسَّعٌ عَلَيْهِ فِي الْآخِرَةِ، وَمَقْتُورٌ عَلَيْهِ فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ، وَمُوَسَّعٌ عَلَيْهِ فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ».

Imepokelewa kutoka kwa Khuraimu Bin Faatik -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Matendo yapo ya aina sita na watu wapo wako aina nne, basi kuna watu wa aina mbili wanaostahiki malipo, na malipo yao huwa sawa na matendo yao, na jema moja hulipwa kwa kumi mfano wake, na jema moja huzidishwa mpaka kufikia mema mia saba, Basi wawili wenye kustahiki malipo ni: Yeyote atakaye kufa hali yakuwa hajamshirikisha Mwenyezi Mungu na kitu chochote ataingia Peponi, na atakaye kufa hali ya kumshirikisha Mwenyezi Mungu na kitu chochote basi ataingia Motoni, na ama yule ambaye atalipwa kwa namna alivyokusudia ni yeyote atakaye kusudia kufanya jambo jema mpaka moyo wake ukahisi kuwa umetenda na Mwenyezi Mungu akajua kutenda kwake huko basi mtu huyo ataandikiwa jema moja, na atakaye fanya kosa ataandikiwa kosa moja, na atakaye fanya jema moja basi hulipwa kwa kumi mfano wake, na mwenye kutoa chochote katika njia ya Mwenyezi Mungu, basi atalipwa kwa kila kimoja kwa mara mia saba, ama watu walivyogawanyika kuna miongoni mwao waliokunjuliwa mambo yao hapa Duniani na wakawa na maisha duni huko Akhera, na kuna wenye maisha Duni hapa duniani na wakakunjuliwa maisha yao huko Akhera, na kuna wenye maisha duni hapa duniani na pia Akhera, na wakakunjuliwa maisha yao hapa duniani na kesho Akhera."

Daraja: Ni nzuri (Hasan)