Hadithi 40 za An-Nawawi · Na. 9
Kutekeleza Amri kwa Uwezo
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ صَخْرٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ: «مَا نَهَيْتُكُمْ عَنْهُ فَاجْتَنِبُوهُ، وَمَا أَمَرْتُكُمْ بِهِ فَأْتُوا مِنْهُ مَا اسْتَطَعْتُمْ، فَإِنَّمَا أَهْلَكَ الَّذِينَ مِنْ قَبْلِكُمْ كَثْرَةُ مَسَائِلِهِمْ وَاخْتِلاَفُهُمْ عَلَى أَنْبِيَائِهِمْ».
Kutoka kwa Abu Hurairah Abdulrahman bin Sakhr (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesema: Nilimsikia Mjumbe wa Allah akisema: "Nililowakataza liepukeni, na nililowaamrisha lifanyeni kulingana na uwezo wenu. Kwani hakika kilichowaangamiza wale waliokuwa kabla yenu ni wingi wa maswali yao yasiyo na maana na kutofautiana kwao na manabii wao."
Daraja: Sahihi