Hadithi 40 za An-Nawawi · Na. 5
Kukataa Uzushi Katika Dini
عَنْ أُمِّ الْمُؤْمِنِينَ أُمِّ عَبْدِ اللَّهِ عَائِشَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهَا قَالَتْ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم: «مَنْ أَحْدَثَ فِي أَمْرِنَا هَذَا مَا لَيْسَ مِنْهُ فَهُوَ رَدٌّ». وفي رواية لمسلم: «مَنْ عَمِلَ عَمَلاً لَيْسَ عَلَيْهِ أَمْرُنَا فَهُوَ رَدٌّ».
Kutoka kwa Mama wa Waumini, Ummu Abdillah Aisha (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesema: Mjumbe wa Allah (Rehema na amani za Allah ziwe juu yake) amesema: "Yeyote atakayezua katika jambo letu hili (dini yetu) lile ambalo halimo ndani yake, basi jambo hilo litakataliwa." Na katika upokezi mwingine wa Muslim: "Yeyote atakayetenda amali yoyote ambayo haina muongozo wetu, basi amali hiyo inakataliwa."
Daraja: Sahihi