Utafiti na Ramani ya Maarifa
UTAFITI

Linganisha Hadith

Ufanano wa maneno: 33%

Ufanano huu unategemea maneno yanayoshirikiana tu. Si hukumu ya kielimu kuhusu maana au daraja la hadith.

Maneno yanayoshirikiana

hamdulillahmwangazaasubuhimizanimbingusadakasubiraradhiimaniardhiswala

Sahih Muslim · Na. 223

Wema, Uadilifu na Tabia Njema

عَنْ أَبِي مَالِكٍ الحَارِثِ بْنِ عَاصِمٍ الأَشْعَرِيِّ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «الطُّهُورُ شَطْرُ الْإِيمَانِ، وَالْحَمْدُ لِلهِ تَمْلَأُ الْمِيزَانَ، وَسُبْحَانَ اللهِ وَالْحَمْدُ لِلهِ تَمْلَآنِ -أَوْ تَمْلَأُ- مَا بَيْنَ السَّمَاءِ وَالأَرْضِ، وَالصَّلَاةُ نُورٌ، وَالصَّدَقَةُ بُرْهَانٌ، وَالصَّبْرُ ضِيَاءٌ، وَالْقُرْآنُ حُجَّةٌ لَكَ أَوْ عَلَيْكَ، كُلُّ النَّاسِ يَغْدُو، فَبَايِعٌ نَفْسَهُ فَمُعْتِقُهَا أَوْ مُوبِقُهَا»

Imepokelea kutoka kwa Abii Maalik Al-Ash-ariy radhi za Mwenyezi Mungu ziwe ju yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake: "Twahara ni nusu ya imani, na kusema Al-hamdulillah neno hilo hujaza mizani, na neno Sub-hanallah neno Alhamdulillah maneno hayo mawili hujaza mizani- au hujaza- sehemu iliyopo kati ya Mbingu na Ardhi, na Swala ni nuru, na sadaka ni dalili ya imani, na subira ni mwangaza, na Qur'ani ni hoja kwako au hoja dhidi yako, watu wote huamka asubuhi na mapema kwa ajili ya kutafuta riziki kuna mwenye huiuza nafasi yake yuko anayeikomboa kutoingia motoni, na miongoni mwao kuna mwenye kuangukia kwenye maasi na akaangamia na kuingia motoni".

Daraja: Sahihi

Hadithi 40 za An-Nawawi · Na. 23

Usafi, Swala, Sadaka na Subira

عَنْ أَبِي مَالِكٍ الْحَارِثِ بْنِ عَاصِمٍ الأَشْعَرِيِّ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم: «الطَّهُورُ شَطْرُ الإِيمَانِ، وَالْحَمْدُ لِلَّهِ تَمْلأُ الْمِيزَانَ، وَسُبْحَانَ اللَّهِ وَالْحَمْدُ لِلَّهِ تَمْلآنِ -أَوْ تَمْلأُ- مَا بَيْنَ السَّمَاءِ وَالأَرْضِ، وَالصَّلاَةُ نُورٌ، وَالصَّدَقَةُ بُرْهَانٌ، وَالصَّبْرُ ضِيَاءٌ، وَالْقُرْآنُ حُجَّةٌ لَكَ أَوْ عَلَيْكَ، كُلُّ النَّاسِ يَغْدُو فَبَائِعٌ نَفْسَهُ فَمُعْتِقُهَا أَوْ مُوبِقُهَا».

Kutoka kwa Abu Malik al-Harith bin Asim al-Ash'ari (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesema: Mjumbe wa Allah amesema: "Usafi ni nusu ya Imani, na Al-hamdulillah inajaza mizani, na Subhanallah na Al-hamdulillah zinajaza kati ya mbingu na ardhi, na Swala ni nuru, na Sadaka ni uthibitisho, na Subira ni mwangaza unaong'aa, na Qur'ani ni hoja ya kukutetea au ya kukuangamiza. Kila mtu asubuhi anatoka kuiuza nafsi yake, ima akaikomboa au akaiangamiza."

Daraja: Sahihi