Utafiti na Ramani ya Maarifa
UTAFITI

Linganisha Hadith

Ufanano wa maneno: 20%

Ufanano huu unategemea maneno yanayoshirikiana tu. Si hukumu ya kielimu kuhusu maana au daraja la hadith.

Maneno yanayoshirikiana

kusuluhishasadakaradhibaina

Jami' at-Tirmidhiy · Na. 2509

Hukumu za Swala na Tohara

عَنْ أَبِي الدَّرْدَاءِ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «أَلاَ أُخْبِرُكُمْ بِأَفْضَلَ مِنْ دَرَجَةِ الصِّيَامِ وَالصَّلاَةِ وَالصَّدَقَةِ؟» قَالُوا: بَلَى، قَالَ: «صَلاَحُ ذَاتِ البَيْنِ، فَإِنَّ فَسَادَ ذَاتِ البَيْنِ هِيَ الحَالِقَةُ».

Kutoka kwa Abuu Dardai -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: "Hivi nisikuelezeni lililo bora kuliko daraja ya swaumu na swala na sadaka?" Wakasema: Tueleze, akasema: "Kusuluhisha kati ya watu, kwani kuharibika kwa mahusiano baina ya watu hilo hunyoa".

Daraja: Sahihi

Hadithi 40 za An-Nawawi · Na. 26

Sadaka ya Kila Kiungo na Kusuluhisha Watu

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم: «كُلُّ سُلاَمَى مِنَ النَّاسِ عَلَيْهِ صَدَقَةٌ كُلَّ يَوْمٍ تَطْلُعُ فِيهِ الشَّمْسُ: تَعْدِلُ بَيْنَ الاثْنَيْنِ صَدَقَةٌ، وَتُعِينُ الرَّجُلَ فِي دَابَّتِهِ فَتَحْمِلُهُ عَلَيْهَا أَوْ تَرْفَعُ لَهُ عَلَيْهَا مَتَاعَهُ صَدَقَةٌ، وَالْكَلِمَةُ الطَّيِّبَةُ صَدَقَةٌ، وَبِكُلِّ خَطْوَةٍ تَمْشِيهَا إِلَى الصَّلاَةِ صَدَقَةٌ، وَتُمِيطُ الأَذَى عَنِ الطَّرِيقِ صَدَقَةٌ».

Kutoka kwa Abu Hurairah (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesema: Mjumbe wa Allah amesema: "Kila kiungo cha binadamu kinawajibika kutolewa sadaka kila siku inayochomoza jua: Kusuluhisha kwa haki baina ya watu wawili ni sadaka, kumsaidia mtu kupanda mnyama wake au kumbebea mzigo wake ni sadaka, neno zuri ni sadaka, kila hatua unayotembea kuelekea kuswali ni sadaka, na kuondoa maudhi njiani ni sadaka."

Daraja: Sahihi