Utafiti na Ramani ya Maarifa
UTAFITI

Linganisha Hadith

Ufanano wa maneno: 15%

Ufanano huu unategemea maneno yanayoshirikiana tu. Si hukumu ya kielimu kuhusu maana au daraja la hadith.

Maneno yanayoshirikiana

shikamanenitahadhariniradhikwani

Sahih al-Bukhari · Na. HE-5504

Wema, Uadilifu na Tabia Njema

عَنْ عَبْدِ اللهِ بنِ مَسعُودٍ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «عَلَيْكُمْ بِالصِّدْقِ، فَإِنَّ الصِّدْقَ يَهْدِي إِلَى الْبِرِّ، وَإِنَّ الْبِرَّ يَهْدِي إِلَى الْجَنَّةِ، وَمَا يَزَالُ الرَّجُلُ يَصْدُقُ وَيَتَحَرَّى الصِّدْقَ حَتَّى يُكْتَبَ عِنْدَ اللهِ صِدِّيقًا، وَإِيَّاكُمْ وَالْكَذِبَ، فَإِنَّ الْكَذِبَ يَهْدِي إِلَى الْفُجُورِ، وَإِنَّ الْفُجُورَ يَهْدِي إِلَى النَّارِ، وَمَا يَزَالُ الرَّجُلُ يَكْذِبُ وَيَتَحَرَّى الْكَذِبَ حَتَّى يُكْتَبَ عِنْدَ اللهِ كَذَّابًا».

Kutoka kwa Abdallah bin Masoud -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: Kutoka kwa Abdillah bin Mas'udi -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Shikamaneni na ukweli, kwani ukweli hupelekea katika wema, na hakika wema hupelekea katika pepo, na hatoacha mtu kuwa mkweli na akishughulika na ukweli mpaka ataandikwa kwa Mwenyezi Mungu kuwa ni mkweli, na tahadharini na uongo, kwani uongo unapelekea katika uovu, na hakika uovu hupelekea katika moto, na hatoacha mtu kuendelea kuwa muongo, na akishughulika na uongo mpaka ataandikwa mbele ya Mwenyezi Mungu kuwa ni muongo".

Daraja: Sahihi

Hadithi 40 za An-Nawawi · Na. 28

Kushikamana na Sunnah na Kuacha Mambo ya Uzushi

عَنْ أَبِي نَجِيحٍ الْعِرْبَاضِ بْنِ سَارِيَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: وَعَظَنَا رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم مَوْعِظَةً وَجِلَتْ مِنْهَا الْقُلُوبُ، وَذَرَفَتْ مِنْهَا الْعُيُونُ، فَقُلْنَا: يَا رَسُولَ اللَّهِ كَأَنَّهَا مَوْعِظَةُ مُوَدِّعٍ فَأَوْصِنَا، قَالَ: «أُوصِيكُمْ بِتَقْوَى اللَّهِ، وَالسَّمْعِ وَالطَّاعَةِ وَإِنْ تَأَمَّرَ عَلَيْكُمْ عَبْدٌ، فَإِنَّهُ مَنْ يَعِشْ مِنْكُمْ فَسَيَرَى اخْتِلاَفاً كَثِيراً، فَعَلَيْكُمْ بِسُنَّتِي وَسُنَّةِ الْخُلَفَاءِ الرَّاشِدِينَ الْمَهْدِيِّينَ، عَضُّوا عَلَيْهَا بِالنَّوَاجِذِ، وَإِيَّاكُمْ وَمُحْدَثَاتِ الأُمُورِ، فَإِنَّ كُلَّ بِدْعَةٍ ضَلاَلَةٌ».

Kutoka kwa Abu Najih Al-Irbadh bin Sariyah (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesema: Mjumbe wa Allah alitupa mawaidha yaliyotikisa nyoyo na yakatiririsha machozi. Tukasema: Ewe Mjumbe wa Allah! Ni kana kwamba haya ni mawaidha ya mtu anayeaga, basi tuusie. Akasema: "Nawausia kumcha Allah, na kusikiliza na kutii hata akitawazwa juu yenu mtumwa. Kwani hakika atakayeishi miongoni mwenu ataona mifarakano mingi. Basi shikamaneni na Sunnah yangu na Sunnah ya Makhalifa waongofu baada yangu, ziumeni kwa meno ya magego, na tahadharini na mambo ya kuzua, kwani kila uzushi ni upotevu."

Daraja: Sahihi