Utafiti na Ramani ya Maarifa
UTAFITI

Linganisha Hadith

Ufanano wa maneno: 39%

Ufanano huu unategemea maneno yanayoshirikiana tu. Si hukumu ya kielimu kuhusu maana au daraja la hadith.

Maneno yanayoshirikiana

tukamshangaaanamuulizakuabudiwaramadhaniakaondokamiongoniunamuonaanakuonatumekaaakawekaviganjauislamuumesemamwenyenyeupenywelenyeusihakunamagotimapaja

Sahih Muslim · Na. 8

Tawhid na Kumtii Mwenyezi Mungu

عن عمر بن الخطاب رضي الله عنه قال: بَيْنَمَا نَحْنُ عِنْدَ رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ ذَاتَ يَوْمٍ إِذْ طَلَعَ عَلَيْنَا رَجُلٌ شَدِيدُ بَيَاضِ الثِّيَابِ، شَدِيدُ سَوَادِ الشَّعَرِ، لَا يُرَى عَلَيْهِ أَثَرُ السَّفَرِ، وَلَا يَعْرِفُهُ مِنَّا أَحَدٌ، حَتَّى جَلَسَ إِلَى النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَأَسْنَدَ رُكْبَتَيْهِ إِلَى رُكْبَتَيْهِ، وَوَضَعَ كَفَّيْهِ عَلَى فَخِذَيْهِ، وَقَالَ: يَا مُحَمَّدُ، أَخْبِرْنِي عَنِ الْإِسْلَامِ، فَقَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «الْإِسْلَامُ أَنْ تَشْهَدَ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ، وَأَنَّ مُحَمَّدًا رَسُولُ اللهِ، وَتُقِيمَ الصَّلَاةَ، وَتُؤْتِيَ الزَّكَاةَ، وَتَصُومَ رَمَضَانَ، وَتَحُجَّ الْبَيْتَ إِنِ اسْتَطَعْتَ إِلَيْهِ سَبِيلًا» قَالَ: صَدَقْتَ، قَالَ: فَعَجِبْنَا لَهُ، يَسْأَلُهُ وَيُصَدِّقُهُ، قَالَ: فَأَخْبِرْنِي عَنِ الْإِيمَانِ، قَالَ: «أَنْ تُؤْمِنَ بِاللهِ، وَمَلَائِكَتِهِ، وَكُتُبِهِ، وَرُسُلِهِ، وَالْيَوْمِ الْآخِرِ، وَتُؤْمِنَ بِالْقَدَرِ خَيْرِهِ وَشَرِّهِ» قَالَ: صَدَقْتَ، قَالَ: فَأَخْبِرْنِي عَنِ الْإِحْسَانِ، قَالَ: «أَنْ تَعْبُدَ اللهَ كَأَنَّكَ تَرَاهُ، فَإِنْ لَمْ تَكُنْ تَرَاهُ فَإِنَّهُ يَرَاكَ» قَالَ: فَأَخْبِرْنِي عَنِ السَّاعَةِ، قَالَ: «مَا الْمَسْؤُولُ عَنْهَا بِأَعْلَمَ مِنَ السَّائِلِ» قَالَ: فَأَخْبِرْنِي عَنْ أَمَارَتِهَا، قَالَ: «أَنْ تَلِدَ الْأَمَةُ رَبَّتَهَا، وَأَنْ تَرَى الْحُفَاةَ الْعُرَاةَ الْعَالَةَ رِعَاءَ الشَّاءِ يَتَطَاوَلُونَ فِي الْبُنْيَانِ» قَالَ: ثُمَّ انْطَلَقَ، فَلَبِثْتُ مَلِيًّا ثُمَّ قَالَ لِي: «يَا عُمَرُ، أَتَدْرِي مَنِ السَّائِلُ؟» قُلْتُ: اللهُ وَرَسُولُهُ أَعْلَمُ، قَالَ: «فَإِنَّهُ جِبْرِيلُ، أَتَاكُمْ يُعَلِّمُكُمْ دِينَكُمْ».

Imepokewa Kutoka kwa Omar bin Khattwab -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Siku moja tukiwa tumekaa kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ghafla akatokea mtu mwenye nguo nyeupe mno, mwenye nywele nyeusi mno, haonekani kuwa na athari yoyote ya safari, na hakuna yeyote amjuaye miongoni mwetu, akaja mpaka akakaa kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, akakunja magoti yake kwa kuyaunganisha na magoti yake mtume (Mithili ya tahiyatu) Na akaweka viganja vyake juu ya mapaja yake, na akasema: Ewe Muhammadi, nieleze kuhusu Uislamu, akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Uislamu ni ushuhudie kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, nakuwa Muhammadi ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na usimamishe sala, na utoe zake, na ufunge Ramadhani, na uhiji katika nyumba tukufu ikiwa utapata uwezo wa kuifikia" Akasema: Sadakta! (Umesema kweli), Anasema: Tukamshangaa: Anamuuliza na anamsadikisha! Akasema: Nieleze kuhusu imani. Akasema: "Nikuwa, umuamini Mwenyezi Mungu, na Malaika wake, na vitabu vyake, na Mitume wake, na siku ya mwisho, na uamini Kadari kheri yake na shari yake" Akasema: Sadakta! (Umesema kweli), akasema: Nieleza kuhusu Ihisani, akasema: "Ni umuabudu Mwenyezi Mungu kana kwamba unamuona, na ikiwa wewe humuoni basi yeye anakuona" Akasema: Nieleze kuhusu Kiyama, akasema: "Muulizwaji si mjuzi sana kama muulizaji" Akasema: Hebu nieleze kuhusu alama zake, akasema: "Ni mjakazi kuzaa bosi wake, na ukiwaona watembea peku, watembea uchi, tena masikini wachunga mbuzi, wakishindana kujenga majengo marefu." (Omar) Akasema: Kisha akaondoka, nikakaa muda mrefu kidogo, kisha Mtume akasema kuniambia: "Ewe Omari, hivi unamjua ni nani muulizaji?" Nikasema: Allah na Mtume wake ndio wajuzi zaidi, akasema: "Huyo ni Jibrili alikuja kukufundisheni dini yenu."

Daraja: Sahihi

Hadithi 40 za An-Nawawi · Na. 2

Nguzo za Uislamu na Imani

عَنْ عُمَرَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ أَيْضاً قَالَ: بَيْنَمَا نَحْنُ جُلُوسٌ عِنْدَ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ذَاتَ يَوْمٍ إِذْ طَلَعَ عَلَيْنَا رَجُلٌ شَدِيدُ بَيَاضِ الثِّيَابِ، شَدِيدُ سَوَادِ الشَّعْرِ، لاَ يُرَى عَلَيْهِ أَثَرُ السَّفَرِ، وَلاَ يَعْرِفُهُ مِنَّا أَحَدٌ، حَتَّى جَلَسَ إِلَى النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم، فَأَسْنَدَ رُكْبَتَيْهِ إِلَى رُكْبَتَيْهِ، وَوَضَعَ كَفَّيْهِ عَلَى فَخِذَيْهِ، وَقَالَ: يَا مُحَمَّدُ أَخْبِرْنِي عَنِ الإِسْلاَمِ؟ فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم: «الإِسْلاَمُ أَنْ تَشْهَدَ أَنْ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَأَنَّ مُحَمَّداً رَسُولُ اللَّهِ، وَتُقِيمَ الصَّلاَةَ، وَتُؤْتِيَ الزَّكَاةَ، وَتَصُومَ رَمَضَانَ، وَتَحُجَّ الْبَيْتَ إِنِ اسْتَطَعْتَ إِلَيْهِ سَبِيلاً» قَالَ: صَدَقْتَ. فَعَجِبْنَا لَهُ يَسْأَلُهُ وَيُصَدِّقُهُ! قَالَ: فَأَخْبِرْنِي عَنِ الإِيمَانِ؟ قَالَ: «أَنْ تُؤْمِنَ بِاللَّهِ، وَمَلاَئِكَتِهِ، وَكُتُبِهِ، وَرُسُلِهِ، وَالْيَوْمِ الآخِرِ، وَتُؤْمِنَ بِالْقَدَرِ خَيْرِهِ وَشَرِّهِ» قَالَ: صَدَقْتَ. قَالَ: فَأَخْبِرْنِي عَنِ الإِحْسَانِ؟ قَالَ: «أَنْ تَعْبُدَ اللَّهَ كَأَنَّكَ تَرَاهُ، فَإِنْ لَمْ تَكُنْ تَرَاهُ فَإِنَّهُ يَرَاكَ»... ثُمَّ انْطَلَقَ فَلَبِثْتُ مَلِيّاً، ثُمَّ قَالَ لِي: «يَا عُمَرُ أَتَدْرِي مَنِ السَّائِلُ؟» قُلْتُ: اللَّهُ وَرَسُولُهُ أَعْلَمُ. قَالَ: «فَإِنَّهُ جِبْرِيلُ أَتَاكُمْ يُعَلِّمُكُمْ دِينَكُمْ».

Kutoka kwa Umar (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesema: Tulipokuwa tumekaa na Mjumbe wa Allah siku moja, alitutokea mtu mwenye nguo nyeupe sana na nywele nyeusi mno, hakuonekana kuwa na alama za msafiri wala hakuna aliyemjua miongoni mwetu. Akaketi mbele ya Mtume akiegemeza magoti yake kwenye magoti yake, na akaweka viganja vyake juu ya mapaja yake, kisha akasema: Ewe Muhammad, nijulishe kuhusu Uislamu? Mtume akasema: 'Uislamu ni kushuhudia kuwa hakuna mungu anayepasa kuabudiwa kwa haki ila Allah na Muhammad ni Mjumbe Wake, kusimamisha Swala, kutoa Zaka, kufunga Ramadhani, na kuhiji Nyumba Tukufu ukiweza njia ya kuelekea huko.' Akasema: 'Umesema kweli.' Tukamshangaa anamuuliza na kumthibitisha! Kisha akauliza kuhusu Imani, akamjibu kuhusu nguzo sita za Imani. Akauliza kuhusu Ihsani, akajibu: 'Ni kumuabudu Allah kana kwamba unamuona, na ikiwa humwoni basi Yeye anakuona.' Kisha yule mtu akaondoka. Baadaye Mtume akasema: 'Huyo alikuwa Jibril, amekuja kuwafundisha dini yenu.'

Daraja: Sahihi