Hivi leo hii nyinyi si mnapata chakula na kinywaji mkitakacho? Kwa hakika mimi nilimuona Nabii wenu rehema na amani ziwe juu yake inafika mahala hapati hata tende mbovu ya kutosha kujaza tumbo lake
Wema, Uadilifu na Tabia Njema
Kiarabu
عَنِ النُّعْمَانِ بْنِ بَشِيرٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: أَلَسْتُمْ فِي طَعَامٍ وَشَرَابٍ مَا شِئْتُمْ؟ لَقَدْ رَأَيْتُ نَبِيَّكُمْ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَمَا يَجِدُ مِنَ الدَّقَلِ مَا يَمْلَأُ بِهِ بَطْنَهُ.
Tafsiri ya Kiswahili
Kutoka kwa Nuuman bin Bashiri radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Hivi leo hii nyinyi si mnapata chakula na kinywaji mkitakacho? Kwa hakika mimi nilimuona Nabii wenu rehema na amani ziwe juu yake inafika mahala hapati hata tende mbovu ya kutosha kujaza tumbo lake.
English translation
An-Nu‘mān ibn Bashīr (may Allah be pleased with him) reported: Are you not (living) in ease, with food and drink as much as you desire? I have seen your Prophet (may Allah's peace and blessings be upon him), and he could not even find low-quality dates to fill his stomach.
Maelezo
Anaeleza Nuuman bin Bashiri radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao, maisha waliyonayo watu miongoni mwa neema, na kwamba wao muda wote wana uhakika wa chakula na kinywaji kwa kiwango watakacho, kisha akaeleza kuhusu hali ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake na kwamba alikuwa hapati katika tende mbovu kiasi cha kujaza tumbo lake kutokana na njaa.
Faida
- Kumebainishwa hali aliyokuwa nayo Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kuipa nyongo Dunia.
- Himizo la kuipa nyongo Dunia, na kuipunguza kwa kadiri iwezekanavyo, na kumuiga Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
- Kuwakumbusha watu neema walizonazo, na kuwahimiza wamshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema hizo.
Jifanyie mazoezi
Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.