Maadili, Adabu na Tabia Njema
SOMO · Sahih al-Bukhari · Na. HE-4243

Amsalimie aliyepanda anayetembea, na anayetembea aliyekaa, na wachache kwa wengi

Wema, Uadilifu na Tabia Njema

Kiarabu

عَن أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «يُسَلِّمُ الرَّاكِبُ عَلَى المَاشِي، وَالمَاشِي عَلَى القَاعِدِ، وَالقَلِيلُ عَلَى الكَثِيرِ». وَلِلبُخَارِي: «يُسَلِّمُ الصَّغِيرُ عَلَى الكَبِيرِ، وَالمَارُّ عَلَى القَاعِدِ، وَالقَلِيلُ عَلَى الكَثِيرِ».

Tafsiri ya Kiswahili

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema: Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Amsalimie aliyepanda anayetembea, na anayetembea aliyekaa, na wachache kwa wengi" Na kwa Bukhari: "Mdogo amsalimie mkubwa, na anayepita amsalimie aliyekaa, na wachache kwa wengi".

English translation

Abu Hurayrah (may Allah be pleased with him) reported that the Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "The one who is riding should greet the one walking, the one who is walking should greet the one sitting, and the small group of people should greet the large one." A version of Al-Bukhāri reads: "The young should greet the old, the passerby should greet the one who is sitting, and the small group of people should greet the larger one."

Maelezo

Ameelekeza Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika adabu za kutoleana salamu kati ya waislamu "Assalaam alaikum warahmatullaahi wabarakaatuh". Mdogo amsalimie mkubwa, na aliyepanda amsalimie anayetembea kwa miguu, na anayetembea kwa mguu amsalimie aliyekaa, na idadi ndogo wawasalimie idadi kubwa.

Faida

  • Sunna ya kutoa salamu kwa mujibu wa yaliyokuja katika hadithi, mtembea kwa miguu anapomsalimia aliyepanda kipando, na wengineo katika hao waliotajwa, inafaa, lakini ni kwenda kinyume na kilicho bora zaidi.
  • Kutoa salamu kwa namna iliyokuja katika hadithi ni katika sababu za mapenzi na kujenga umoja.
  • Wakiwa wanalingana na wako sawa katika hayo yaliyotajwa, basi mbora wao ni yule atakayeanza kwa salamu.
  • Ukamilifu wa sheria hii katika kubainisha yote anayoyahitaji mwanadam.
  • Kufundisha adabu za salamu na kumpa kila mwenye haki haki yake.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)