Fiqhi, Swala na Ibada
SOMO · Sahih Muslim · Na. HE-4198

Atakayeswali (wakati) wa baridi mbili ataingia peponi

Hukumu za Swala na Tohara

Kiarabu

عن أَبِي مُوسَى الأَشْعَرِيِّ رضي الله عنه: أَنَّ رَسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ: «مَنْ صَلَّى ‌الْبَرْدَيْنِ دَخَلَ الْجَنَّةَ»

Tafsiri ya Kiswahili

Imepokelewa Kutoka kwa Abuu Musa Al-Ash'ariy -Radhi za Allah ziwe juu yake- ya kwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakayeswali (wakati) wa baridi mbili ataingia peponi"

English translation

Abu Mūsa al-Ash‘ari (may Allah be pleased with him) reported: The Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "Whoever prays the Bardayn (Fajr and ‘Asr prayers) will enter Paradise."

Maelezo

Mtume rehema na amani ziwe juu yake amehimiza kufanya bidii katika kuswali Swala mbili za nyakati za baridi, ambazo ni sala ya Alfajiri na Alasiri, na akawabashiria kuwa mwenye kutekeleza haki zake kwa muda, na kwa jamaa na mambo mengine, basi zitakuwa ni sababu ya kuingia kwake Peponi.

Faida

  • Fadhila ya kuhifadhi Sala ya Alfajiri na Alasiri; Kwa sababu Alfajiri ni wakati wa usingizi mzuri, na Alasiri ni wakati mtu anashughulika na kazi zake, basi atakayezihifadhi atakuwa na haki zaidi ya kuzihifadhi Swala zilizosalia.
  • Sala ya Alfajiri na Alasiri zimeitwa baridi mbili; Kwa sababu Swala ya Alfajiri ina ubaridi wa usiku, na Sala ya Alasiri ina ubaridi wa mchana, hata ikiwa ni katika wakati wa joto, ni nyepesi kuliko wakati wa kabla yake, au zimeitwa hivyo kwa kuzingatia kawaida ya nyakati nyingi huwa hivyo, kama ambavyo husemwa: Miezi miwili, kwa kumaanisha jua na mwezi.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)