Yeyote atakayenidhaminia mimi vilivyo kati ya Taya mbili na vilivyo kati ya miguu yake ninampa dhamana ya Pepo
Wema, Uadilifu na Tabia Njema
Kiarabu
عن سهل بن سعد رضي الله عنه عن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: «مَنْ يَضْمَنْ لِي مَا بَيْنَ لَحْيَيْهِ وَمَا بَيْنَ رِجْلَيْهِ أَضْمَنْ لَهُ الْجَنَّةَ».
Tafsiri ya Kiswahili
Imepokelewa Kutoka kwa Sahal Ibn Sa'd -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Yeyote atakayenidhaminia mimi vilivyo kati ya Taya mbili na vilivyo kati ya miguu yake ninampa dhamana ya Pepo".
English translation
Sahl ibn Sa‘d (may Allah be pleased with him) reported: The Messenger of Allah (may Allah’s peace and blessings be upon him) said: "Whoever gives me a guarantee to safeguard what is between his jaws and what is between his legs, I will guarantee him Paradise."
Maelezo
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu mambo mawili nayo muislamu basi ataingia Peponi, La kwanza: Kuhifadhi ulimi kutozungumza yale yenye kumchukiza Allah Mtukufu, La pili: Kuhifadhi tupu kutotumbukia katika machafu; Kwa sababu viungo viwili hivi hukithiri kutokea maasi kwavyo.
Faida
- Kuhifadhi ulimi na tupu ni njia ya kuingia Peponi.
- Umetajwa mahususi ulimi na utupu; kwa sababu ndio vyanzo vikuu vya balaa kwa mwanadamu katika dunia na Akhera.
Jifanyie mazoezi
Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.