Qur'ani Tukufu na Fadhila Zake
SOMO · Sahih al-Bukhari · Na. 4772

Ewe baba yangu mdogo, sema: Laa ilaaha illa llaahu (Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu) neno ambalo nitakutetea kwalo mbele ya Mwenyezi Mungu

Usomaji na Kufanyia Kazi Qur'ani

Kiarabu

عن سَعِيدِ بْنِ الْمُسَيَّبِ، عَنْ أَبِيهِ قَالَ: لَمَّا حَضَرَتْ أَبَا طَالِبٍ الْوَفَاةُ، جَاءَهُ رَسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم فَوَجَدَ عِنْدَهُ أَبَا جَهْلٍ وَعَبْدَ اللهِ بْنَ أَبِي أُمَيَّةَ بْنِ الْمُغِيرَةِ، فَقَالَ: «أَيْ عَمِّ، قُلْ: لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ، كَلِمَةً أُحَاجُّ لَكَ بِهَا عِنْدَ اللهِ»، فَقَالَ أَبُو جَهْلٍ وَعَبْدُ اللهِ بْنُ أَبِي أُمَيَّةَ: أَتَرْغَبُ عَنْ مِلَّةِ عَبْدِ الْمُطَّلِبِ، فَلَمْ يَزَلْ رَسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم يَعْرِضُهَا عَلَيْهِ، وَيُعِيدَانِهِ بِتِلْكَ الْمَقَالَةِ، حَتَّى قَالَ أَبُو طَالِبٍ آخِرَ مَا كَلَّمَهُمْ: عَلَى مِلَّةِ عَبْدِ الْمُطَّلِبِ، وَأَبَى أَنْ يَقُولَ: لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم: «وَاللهِ لَأَسْتَغْفِرَنَّ لَكَ مَا لَمْ أُنْهَ عَنْكَ»، فَأَنْزَلَ اللهُ: {مَا كَانَ لِلنَّبِيِّ وَالَّذِينَ آمَنُوا أَنْ يَسْتَغْفِرُوا لِلْمُشْرِكِينَ} [التوبة: 113]، وَأَنْزَلَ اللهُ فِي أَبِي طَالِبٍ، فَقَالَ لِرَسُولِ اللهِ صلى الله عليه وسلم: {إِنَّكَ لا تَهْدِي مَنْ أَحْبَبْتَ وَلَكِنَّ اللهَ يَهْدِي مَنْ يَشَاءُ} [القصص: 56].

Tafsiri ya Kiswahili

Kutoka kwa Saidi Bin Musayyab, kutoka kwa baba yake amesema: Yalipomfika mauti Abuu Twalib, Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alimjia akamkuta yuko pamoja na Abuu Jahali na Abdallah Bin Umaiyya bin Mughiira, akasema: "Ewe baba yangu mdogo, sema: Laa ilaaha illa llaahu (Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu) neno ambalo nitakutetea kwalo mbele ya Mwenyezi Mungu", Abuu Jahali akasema: Hivi unataka kuichukia mila ya Abdul Muttwalib (Yaani baba yake) Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akaendelea kumrejelea neno hilo, nao pia wakirudia kumwambia maneno yao, mpaka Abuu Twalib akasema kwa neno lake la mwisho alilowasemesha: Niko katika mila ya Abdul Muttwalib, na akakataa kusema: Laa ilaaha illa llaah, mpokezi anasema: Akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Wallahi (Namuapia Allah) nitakuombea msamaha kwa muda wote madam sijakatazwa, Allah akateremsha: "Haifai wala haitakiwi kwa Nabii na wale walioamini kuwaombea msamaha washirikina" [Attauba: 113], Na akateremsha kuhusu Abuu Twalib, akasema kumwambia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Hakika wewe humuongoi umpendaye, lakini Allah anamuongoa amtakaye" [Al-Qasas:56]

English translation

Sa‘īd ibn al-Musayyab reported that his father said: When Abu Tālib was about to die, the Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) came to him and found Abu Jahl and 'Abdullah ibn Abi' Umayyah ibn al-Mughīrah with him. He said: "O uncle, say: La ilāha illallāh (there is no god but Allah), a word with which I can defend you before Allah." Abu Jahl and 'Abdullah ibn Abi' Umayyah said: Would you abandon the religion of 'Abdul-Muttalib? The Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) kept repeating his request, and they also kept repeating their words to him. The last thing Abu Tālib said to them was: On the religion of 'Abdul-Muttalib, refusing to say: There is no god but Allah. He said: The Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "By Allah, I shall continue seeking forgiveness for you unless I am forbidden from doing so." So Allah revealed: {It is not fitting for the Prophet and those who believe in seeking forgiveness for the polytheists.} [Surat at-Tawbah: 113]. Allah also revealed regarding Abu Tālib and addressing the Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him): {You cannot guide whoever you like, but Allah guides whom He wills.} [Surat al-Qasas: 56]

Maelezo

Aliingia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kwa Ami yake Abuu Twalib akiwa katika hali ya kukaribia kufa, akasema kumwambia: Ewe Ami yangu sema "Laa ilaaha illa llaah", neno ambalo nitakutolea ushahidi kwalo mbele ya Allah, Abuu Jahali na Abdallah Bin Abiiy Umaiyya wakasema: "Wewe Abuu Twalib!, unaacha mila ya baba yako Abdul Muttwalib?! ambayo ni kuabudu masanamu, wakaendelea kumwambia hivyo mpaka akasema neno lake la mwisho alilowaambia kuwa: Niko katika mila ya Abdul Muttwalib, mila ya ushirikina na kuabudu masanamu, Akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: Nitakuombea msamaha madam sijakatazwa na Mola wangu kuhusu hilo, ikateremka kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Haipasi kwa Nabii na wale walioamini kuwatakia msamaha washirikina, hata kama watakuwa ni jamaa zao, baada ya kwisha bainika kuwa hao ni watu wa Motoni" [Attauba: 113], Na ikateremka kumuhusu Abuu Twalib kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Hakika wewe, humuongoi, unayependa aongoke. Lakini Mwenyezi Mungu, Anamuongoa Anayemtaka. Na Yeye Ndiye Anayemjua zaidi anayefaa kuongoka". Kwani hakika wewe humuongoi umpendaye kumuongoa, bali jukumu lako ni kufikisha, na Allah anamuongoa amtakaye.

Faida

  • Uharamu wa kuwaombea msamaha washirikina vyovyote vile utakavyokuwa ukaribu wao na matendo yao na wema wao.
  • Kuwaiga mababa na wazee katika batili ni katika vitendo vya watu wa zama za ujinga.
  • Ukamilifu wa huruma yake Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- na pupa yake katika kuwalingania watu na kuwaongoza.
  • Hili ni jibu kwa watu wanaodai kuwa Abuu Twalib alisilimu.
  • Matendo huzingatiwa mwisho.
  • Kubatilika kujifungamanisha na kushikamana na Mtume au mwingine asiyekuwa yeye kwa lengo la kupata kheri na kuzuia madhara.
  • Atakayesema "Laa ilaaha illa llaah" kwa kuwa na elimu na yakini na kuitakidi kwa dhati juu yake basi atakuwa kaingia ndani ya Uislamu.
  • Madhara ya watu waovu na marafiki wabaya kwa mwanadam.
  • Maana ya "Laa ilaaha illa llaah": Ni kuacha ibada za masanamu na wachamungu na watu wema na kumpwekeshea ibada Mwenyezi Mungu peke yake, nakwamba washirikina wanaju maana yake.
  • Inafaa kumtembelea mgonjwa mshirikina ikiwa anatarajiwa huenda akasilimu.
  • Uongofu wa kumuafikisha mja afungue moyo wake uko mkononi mwa Allah peke yake hana mshirika, bali jukumu la Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ni kuongoza kwa kuelekeza, muongozo, na kufikisha ujumbe.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)