Hakika katika watu waovu zaidi ni wale watakaokutwa na Kiyama wakiwa hai, na mwenye kuyafanya makaburi kuwa mahala pa kusalia
Tawhid na Kumtii Mwenyezi Mungu
Kiarabu
عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بن مسعودٍ رضي الله عنه قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: «إِنَّ مِنْ شِرَارِ النَّاسِ مَنْ تُدْرِكُهُ السَّاعَةُ وَهُمْ أَحْيَاءٌ، وَمَنْ يَتَّخِذُ الْقُبُورَ مَسَاجِدَ».
Tafsiri ya Kiswahili
Kutoka kwa Abdallah bin Masoud -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Hakika katika watu waovu zaidi ni wale watakaokutwa na Kiyama wakiwa hai, na mwenye kuyafanya makaburi kuwa mahala pa kusalia".
English translation
‘Abdullah ibn Mas‘ūd (may Allah be pleased with him) reported that he heard the Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) say: "Among the most wicked people are those who will be alive when the Hour comes, and those who take the graves as places of worship."
Maelezo
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu watu waovu, nakuwa hao ndio Kiyama kitasimama juu yao, na wale wanaoyafanya makaburi kuwa misikiti, wakisali hapo na wakiyaelekea wakati wa ibada.
Faida
- Uharamu wa kujenga misikiti juu ya makaburi; kwa sababu kitendo hicho ni njia ya kuingia katika shirki.
- Uharamu wa kusali katika makaburi hata bila kujengea; kwa sababu msikiti ni jina la kila mahali panaposujudiwa hapo hata kama hakuna jengo.
- Atakayeyafanya makaburi ya watu wema kuwa mahala pa kusalia huyo ni katika viumbe waovu, hata kama atadai kuwa lengo lake ni kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Jifanyie mazoezi
Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.