Maadili, Adabu na Tabia Njema
SOMO · Sahih Muslim · Na. 54

Hamtoingia peponi mpaka muamini, na hamtoamini mpaka mpendane, je nisikufahamisheni juu ya jambo ambalo mkilifanya mtapendana? toleaneni salamu kwa wingi kati yenu

Wema, Uadilifu na Tabia Njema

Kiarabu

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «لَا تَدْخُلُونَ الْجَنَّةَ حَتَّى تُؤْمِنُوا، وَلَا تُؤْمِنُوا حَتَّى تَحَابُّوا، أَوَلَا أَدُلُّكُمْ عَلَى شَيْءٍ إِذَا فَعَلْتُمُوهُ تَحَابَبْتُمْ؟ أَفْشُوا السَّلَامَ بَيْنَكُمْ».

Tafsiri ya Kiswahili

Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -sala na amani ziwe juu yake-: "Hamtoingia peponi mpaka muamini, na hamtoamini mpaka mpendane, je nisikufahamisheni juu ya jambo ambalo mkilifanya mtapendana? toleaneni salamu kwa wingi kati yenu".

English translation

Abu Hurayrah (may Allah be pleased with him) reported that the Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "You will not enter Paradise until you believe and you will not believe until you love one another. Shall I guide you to something which, if you do, you will love one another? Spread the greeting of peace among yourselves."

Maelezo

Amebainisha Mtume Rehema na amani ziwe juu yake yakuwa hatoingia peponi ila muumini, na wala haikamiliki imani na wala haitengemai hali ya jamii ya kiislamu mpaka wapendane baina yao. Kisha akaelekeza Mtume Rehema na amani ziwe juu yake katika jambo muhimu zaidi ambalo litaleta mapenzi kwa wote, nalo ni waislamu kutoleana salam baina yao, aliyoifanya Mwenyezi Mungu kuwa ni salam kwa waja wake.

Faida

  • Kuingia peponi hakui ila kwa imani.
  • Katika ukamilifu wa imani ni muislamu kumpendelea muislamu mwenzake yale anayoyapenda yeye.
  • Ni sunna kutoa salam na kuisambaza kwa waislamu; kwa sababu kuisambaza ni kusambaza mapenzi na amani baina ya watu.
  • Salam haitolewi ila kwa muislamu; kwa kauli yake Rehema na amani ziwe juu yake: "Baina yenu".
  • Kutoa salam kunaondoa chuki na kuhamana na vifundo.
  • Umuhimu wa mapenzi kati ya waislamu nakuwa hilo ni katika ukamilifu wa imani.
  • Imekuja katika hadithi nyingine kuwa namna ya salam kamili ni: "As-salaam alaikum warahmatullahi wabarakaatuh", na inatosha: "Assalaam alaikum".

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)