Bukhari — bado haijapangwa (ya muda)
SOMO · Sahih al-Bukhari · Na. 206

Ziache, kwani hakika mimi nimezivaa zikiwa safi

Hadith zilizogunduliwa hivi karibuni (ya muda)

Kiarabu

عَنْ المُغِيرَةِ رضي الله عنه قَالَ: كُنْتُ مَعَ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي سَفَرٍ، فَأَهْوَيْتُ لِأَنْزِعَ خُفَّيْهِ، فَقَالَ: «دَعْهُمَا، فَإِنِّي أَدْخَلْتُهُمَا طَاهِرَتَيْنِ» فَمَسَحَ عَلَيْهِمَا.

Tafsiri ya Kiswahili

Kutoka kwa MughIira Radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Nilikuwa pamoja na Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- katika safari, nikanyoosha mikono ili nimvue viatu vyake (khufu), akasema: "Ziache, kwani hakika mimi nimezivaa zikiwa safi", akafuta juu yake.

English translation

Al-Mughīrah (may Allah be pleased with him) reported: Once I was in the company of the Prophet (may Allah's peace and blessings be upon him) on a journey and I bent down to take off his leather socks, but he said: "Leave them, for I had put them on when they were in the state of purity." So, he wiped over them.

Maelezo

Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- katika moja ya safari zake akatawadha, alipofikia kuosha miguu miwili alinyoosha Mughira bin Shu'ba Radhi za Allah ziwe juu yake mikono yake ili avue kilichokuwa miguuni kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- katika khufu (viatu mithili ya soksi) ili Mtume aoshe miguu yake! Akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: Ziache na wala usizivue, kwani mimi niliingiza miguu yangu ndaniya khufu mbili nikiwa katika twahara, Akafuta Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- juu ya khufu zake badala ya kuosha miguu miwili.

Faida

  • Sheria ya kufuta juu ya khufu mbili inakuwa wakati wa kutia udhu kwa ajili ya hadathi ndogo, ama kuoga kwa ajili ya hadathi kubwa ni lazima kuosha miguu.
  • Kufuta kunakuwa mara moja kwa kupitisha mkono ulioloana juu ya khufu nasi chini yake.
  • Ni sharti wakati wa kufuta juu ya khufu iwe kuzivaa kwake ni baada ya udhu kamili ambao aliosha miguu yake wakati huo kwa maji, na khufu ziwe twahara (safi) na zifunike mahali panapolazimika kuoshwa katika miguu, na kuwe kufuta ni katika hadathi ndogo si katika janaba au chochote kinachowajibisha kuoga, na kufuta kuwe katika muda uliopangwa kisheria nao ni usiku na mchana kwa mwenyeji na siku tatu kwa msafiri.
  • Kitapimwa katika khufu mbili kila chenye kusitiri miguu miwili kama soksi na kinginecho, inafaa kufuta juu yake.
  • Uzuri wa tabia za Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- na mafundisho yake, kiasi kwamba alimzuia Mughira kumvua, na akamueleza sababu: Kuwa alizivaa akiwa twahara; ili nafsi yake itulizane, na ajue hukumu ya hilo.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)