Bukhari — bado haijapangwa (ya muda)
SOMO · Sahih al-Bukhari · Na. 611

Mtakaposikia wito (Adhana), basi semeni mfano wa yale ayasemayo muadhini

Hadith zilizogunduliwa hivi karibuni (ya muda)

Kiarabu

عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الخُدْرِيِّ رضي الله عنه أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «إِذَا سَمِعْتُمُ النِّدَاءَ، فَقُولُوا مِثْلَ مَا يَقُولُ المُؤَذِّنُ».

Tafsiri ya Kiswahili

Kutoka kwa Abuu Saidi Al-Khudry -Radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Mtakaposikia wito (Adhana), basi semeni mfano wa yale ayasemayo muadhini".

English translation

Abu Sa‘īd al-Khudri (may Allah be pleased with him) reported that the Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "When you hear the Adhan (call to prayer), repeat what the Muezzin says."

Maelezo

Anahimiza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kumjibu muadhini wakati wa kumsikia, na hii ni kwa sisi kusema mfano wa ayasemayo, sentensi kwa sentensi, Anaposema Allaahu Akbaru nasi tunasema Allaahu Akbaru, na anapotamka shahada mbili, nasi tunazitamka baada yake, Linaondolewa tamko la: (Hayya a'las swalaa, Hayya a'lal falaah) hapo tutasema baada yake: Laa haulaa walaa quwwata illaa billaah.

Faida

  • Atamfuatisha muadhini wa kwanza baada ya kumaliza wa kwanza, hata kama waadhini watakuwa wengi; kwa sababu ya ujumla wa hadithi hii.
  • Atamjibu muadhini katika hali zake zote, ikiwa atakuwa hayuko chooni au akikidhi haja.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)