Aqidah na Misingi ya Imani
SOMO · Sunan Abu Dawud · Na. 4833

Mtu huwa katika mwenendo wa rafiki yake wa karibu, basi na aangalie mmoja wenu ni nani anayemfanya kuwa rafiki yake

Tawhid na Kumtii Mwenyezi Mungu

Kiarabu

عن أبي هريرة رضي الله عنه أَن النبيَّ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم قَالَ: «الرَّجُلُ عَلَى دِينِ خَلِيلِهِ، فَلْيَنْظُر أَحَدُكُم مَنْ يُخَالِل».

Tafsiri ya Kiswahili

Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake: Kuwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- Amesema: "Mtu huwa katika mwenendo wa rafiki yake wa karibu, basi na aangalie mmoja wenu ni nani anayemfanya kuwa rafiki yake"

English translation

Abu Hurayrah (may Allah be pleased with him) reported: The Prophet (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "A man follows the religion (i.e. ways and manners) of his close friend. So, each of you should carefully consider whom he takes as his intimate friend."

Maelezo

Alibainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa mtu hufanana na rafiki na jamaa yake wa dhati katika nyenendo na tabia zake, na urafiki huathiri maadili, tabia na matendo, na kwa ajili hiyo alielekeza vyema katika uchaguzi wa rafiki. Kwa sababu atamuongoza rafiki yake katika imani na uongofu na kheri, na atakuwa ni msaada kwa rafiki yake.

Faida

  • Amri ya kusuhubiana na wema na kuwachambua, na katazo la kusuhubiana na watu wabaya.
  • Ametajwa rafiki badala ya ndugu; Kwa sababu wewe ndiye unayemchagua rafiki, lakini ndugu na jamaa, huna chaguo.
  • Kumchukua mtu kuwa rafiki lazima kuanze na kutafakari.
  • Mtu huiimarisha dini yake kwa kusuhubiana na waumini na huidhoofisha kusuhubiana na watu waovu.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)