Fiqhi, Swala na Ibada
SOMO · Sahih Muslim · Na. 273

Nilikuwa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake akafika katika jalala la watu fulani akakidhi haja ndogo akiwa kasimama,

Hukumu za Swala na Tohara

Kiarabu

عَنْ حُذَيْفَةَ رضي الله عنه قَالَ: كُنْتُ مَعَ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَانْتَهَى إِلَى سُبَاطَةِ قَوْمٍ، فَبَالَ قَائِمًا، فَتَنَحَّيْتُ فَقَالَ: «ادْنُهْ» فَدَنَوْتُ حَتَّى قُمْتُ عِنْدَ عَقِبَيْهِ فَتَوَضَّأَ فَمَسَحَ عَلَى خُفَّيْهِ.

Tafsiri ya Kiswahili

Kutoka kwa Hudhaifa -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilikuwa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake akafika katika jalala la watu fulani akakidhi haja ndogo akiwa kasimama, nikasimama kando naye, alipomaliza akasema: “Sogea karibu” nikasogea mpaka nikasimama karibu naye, akatawadha, kisha akapangusa juu ya soksi (Khufu) zake.

English translation

Hudhayfah (may Allah be pleased with him) reported: I was with the Prophet (may Allah's peace and blessings be upon him) when he arrived at the dump of some people and passed urine while standing. I stepped aside, but he said: "Draw near." So, I drew near until I stood behind his heels, and he performed ablution and wiped over his leather socks.

Maelezo

Imepokelewa kutoka kwa Hudhaifa bin Al-Yaman kwamba alikuwa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akataka kukidhi haja ndogo, akaingia dampo la watu fulani; Napo ni mahali ambapo takataka na uchafu unaofagiliwa kutoka majumbani hutupwa hapo, hivyo akakidhi haja ndogo akiwa kasimama, na huwa anakidhi haja ndogo akiwa kachuchumaa. Basi Hudhaifa akajisogeza mbali naye, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamwambia: Njoo karibu, basi Hudhaifa akamkaribia mpaka akasimama nyuma yake, nyuma ya miguu yake; Ili awe kama mstara kwake kutokana na watu kumtazama katika hali ile. Kisha akatawadha, rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, na wakati wa kuosha miguu yake, alitosheka kwa kupangusa juu ya soksi (Khofu) zake - nazo ni zile zinazovaliwa miguuni, zilizotengenezwa kwa ngozi nyembamba na mfano wake na zinazofunika vifundo vya miguu, na wala hakuzivua.

Faida

  • Sheria ya kupangusa juu ya Khufu (Soksi) mbili.
  • Inafaa kukidhi haja wima, kwa sharti asidondokewe na chochote.
  • Mtume rehema na amani ziwe juu yake, alichagua Jalala, ambapo ni mahali pa kutupia taka za wafagiaji, kwa sababu huwa ni rahisi, na haja ndogo huwa hairudi tena kwa mkojoaji.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)