Fiqhi, Swala na Ibada
SOMO · Sahih Muslim · Na. 433

Nyoosheni safu zenu, kwani hakika kunyoosha safu ni katika ukamilifu wa swala

Hukumu za Swala na Tohara

Kiarabu

عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «سَوُّوا صُفُوفَكُمْ، فَإِنَّ تَسْوِيَةَ الصَّفِّ مِنْ تَمَامِ الصَّلَاةِ».

Tafsiri ya Kiswahili

Imepokelewa kutoka kwa Anas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake: "Nyoosheni safu zenu, kwani hakika kunyoosha safu ni katika ukamilifu wa swala"

English translation

Anas ibn Mālik (may Allah be pleased with him) reported: The Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "Straighten your rows, for indeed, straightening the row is from the perfection of the prayer."

Maelezo

Anawaamrisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake wenye kuswali kunyoosha safu zao, na wasitanguliane wala wasirudi nyuma, na kwamba kuzinyoosha ni sehemu ya kukamilisha na ukamilifu wa Sala, na kuwa kupinda kwa safu ni dosari na ni upungufu ndani yake.

Faida

  • Sheria ya kuchunga kila kinachokamilisha swala na kuiweka mbali na upungufu.
  • Hekima ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika kufundisha, kwani aliihusisha hukumu na sababu yake; ili iwe wazi hekima ya kuletwa sheria hiyo, na nafsi ipate hamasa ya kuitekeleza.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)