Aqidah na Misingi ya Imani
SOMO · Sahih al-Bukhari · Na. HE-2945

Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu anakukatazeni kuapa kwa baba zenu

Tawhid na Kumtii Mwenyezi Mungu

Kiarabu

عَنْ عُمَرَ بْنِ الْخَطَّابِ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «إِنَّ اللهَ عَزَّ وَجَلَّ يَنْهَاكُمْ أَنْ تَحْلِفُوا بِآبَائِكُمْ»، قَالَ عُمَرُ: فَوَاللهِ مَا حَلَفْتُ بِهَا مُنْذُ سَمِعْتُ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ نَهَى عَنْهَا ذَاكِرًا وَلَا آثِرًا.

Tafsiri ya Kiswahili

Imepokewa kutoka kwa Omar Bin Khattwab- Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- "Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu anakukatazeni kuapa kwa baba zenu", akasema Omari: Wallahi sikuwahi kuapa tena kwa kiapo hicho tangu nilipomsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alipokataza hivyo, kwa kutamka mwenyewe wala kwa kunukuu kiapo cha mtu mwingine.

English translation

‘Umar ibn al-Khattāb (may Allah be pleased with him) reported that the Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "Indeed, Allah Almighty forbids you to swear by your forefathers." ‘Umar said: By Allah, I have never sworn by that since I heard that the Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) forbade it, neither deliberately nor reporting it from others.

Maelezo

Ameeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu anakataza kuapa kwa baba, atakayetaka kuapa basi asiape ila kwa jina la Mwenyezi Mungu, na wala asiape kwa jina la mwingine. Kisha Omari bin Khattwab radhi za Allah ziwe juu yake akaeleza kuwa hakuwahi tena kuapa tangu alipomsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akikataza kufanya hivyo, si kwa makusudi wala kwa kunukuu kiapo cha mtu mwingine aliyeapa kinyume na Mwenyezi Mungu.

Faida

  • Uharamu wa kuapia kinyume na Mwenyezi Mungu, na kataja kumwapia baba kwa sababu hii ilikuwa ni katika desturi za zama za ujinga.
  • Kiapo: Ni kuapa kwa jina la Mwenyezi Mungu au kwa majina yake au sifa zake katika jambo miongoni mwa mambo kwa ajili kutilia mkazo.
  • Ubora wa Omari radhi za Allah ziwe juu yake kwa wepesi wake wa kutekeleza na uzuri wa uelewa wake na unyenyekevu wake.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)