Atakaye hiji kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na hakufanya matendo mabaya,na hakufanya uwovu, atarudi kama siku aliyozaliwa na mama yake
Hukumu za Swala na Tohara
Kiarabu
عن أبي هريرة رضي الله عنه قال: سمعت النبي صلى الله عليه وسلم يقول: «مَنْ حَجَّ لِلهِ فَلَمْ يَرْفُثْ وَلَمْ يَفْسُقْ رَجَعَ كَيَوْمِ وَلَدَتْهُ أُمُّهُ».
Tafsiri ya Kiswahili
Imepokelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi mungu ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Atakaye hiji kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na hakufanya matendo mabaya,na hakufanya uwovu, atarudi kama siku aliyozaliwa na mama yake"
English translation
Abu Hurayrah (may Allah be pleased with him) reported: I heard the Messenger of Allah (may Allah’s peace and blessings be upon him) say: "Whoever performs Hajj without engaging in rafath (sexual relations or obscene speech) or sinning will return like the day his mother gave birth to him."
Maelezo
Anaweka wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakaye hiji kwa kutaka radhi za Allah Mtukufu na akawa hakufanya yasiyofaa; Na yasiyofaa hapa maana yake ni tendo la ndoa na vitangulizi vyake, kama busu, kugusana, neno hili hutumika pia kumaanisha maneno machafu, na akawa hakufanya uovu; kwa kufanya maasi na madhambi, Na miongoni mwa uovu ni kufanya makatazo ya ihiramu (Hija), atarudi kutoka katika hija yake akiwa kasamehewa, kama azaliwavyo mtoto akiwa amesalimika kutokana na madhambi.
Faida
- Uwovu pamoja na kuwa umekatazwa katika hali zote, katazo hilo linatiwa mkazo katika Hija kwa kuheshimu na kutukuza ibada ya Hija.
- Mwanadamu huzaliwa pasina kuwa na makosa akiwa kaepukana na madhambi; hivyo hawezi kubeba madhambi ya mwingine.
Jifanyie mazoezi
Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.