Usimuue, kwani ukimuuua basi yeye atakuwa katika nafasi yako kabla hujamuua, na wewe utakuwa katika nafasi yake kabla hajasema neno lake alilolisema
Tawhid na Kumtii Mwenyezi Mungu
Kiarabu
عَنْ المِقْدَادِ بْنَ عَمْرٍو الكِنْدِيَّ رضي الله عنه: أَنَّهُ قَالَ لِرَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: أَرَأَيْتَ إِنْ لَقِيتُ رَجُلًا مِنَ الكُفَّارِ فَاقْتَتَلْنَا، فَضَرَبَ إِحْدَى يَدَيَّ بِالسَّيْفِ فَقَطَعَهَا، ثُمَّ لاَذَ مِنِّي بِشَجَرَةٍ، فَقَالَ: أَسْلَمْتُ لِلَّهِ، أَأَقْتُلُهُ يَا رَسُولَ اللَّهِ بَعْدَ أَنْ قَالَهَا؟ فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «لاَ تَقْتُلْهُ» فَقَالَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ إِنَّهُ قَطَعَ إِحْدَى يَدَيَّ، ثُمَّ قَالَ ذَلِكَ بَعْدَ مَا قَطَعَهَا؟ فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «لاَ تَقْتُلْهُ، فَإِنْ قَتَلْتَهُ فَإِنَّهُ بِمَنْزِلَتِكَ قَبْلَ أَنْ تَقْتُلَهُ، وَإِنَّكَ بِمَنْزِلَتِهِ قَبْلَ أَنْ يَقُولَ كَلِمَتَهُ الَّتِي قَالَ».
Tafsiri ya Kiswahili
Kutoka kwa Mikidadi bin Amri Al-Kindi radhi za Allah ziwe juu yake: Ya kwamba yeye alisema kumuuliza Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- Unaonaje ikiwa nitakutana na mtu miongoni mwa makafiri, tukapigana, akapiga moja ya mikono yangu kwa upanga akaukata, kisha akajificha katika mti, akasema: Nimejisalimisha kwa Mwenyezi Mungu, je nimuue ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu baada ya kuwa amelisema neno hilo? Akasema: "Usimuue" Nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu kakata moja ya mikono yangu, Kisha akasema hivyo baada ya kuwa kaukata?! Akasema: "Usimuue, kwani ukimuuua basi yeye atakuwa katika nafasi yako kabla hujamuua, na wewe utakuwa katika nafasi yake kabla hajasema neno lake alilolisema".
English translation
Al-Miqdād ibn ‘Amr al-Kindi (may Allah be pleased with him) reported: He said to the Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him): What if I meet a man from the disbelievers and we both fight? He strikes one of my hands with the sword and cuts it off, then he seeks refuge from me in a tree and says: I have submitted to Allah. O Messenger of Allah, should I kill him after saying it? The Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "Do not kill him." He said: O Messenger of Allah, he cut off one of my hands, then he said this after cutting it off. The Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "Do not kill him, for if you kill him, he will be in the same position as yours before you kill him, and you will be in the same position as his before saying the word that he said."
Maelezo
Mikidadi bin Aswadi radhi za Allah ziwe juu yake alimuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake pindi atakapokutana na mtu miongoni mwa makafiri katika mapambano, wakapambana kwa mapanga, mpaka yule kafiri akakata mmoja kati ya mikono yake kwa upanga, kisha kafiri akamkimbia na akajikinga katika mti, akasema: Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, je, ni halali kwangu kumuua baada yakuwa amekata mkono wangu? Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamwambia: Hapana, usimuuwe. Akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, lakini yeye kakata moja ya mikono yangu, pamoja na hivyo bado tu nisimuuwe?! Akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Hapana, usimuuwe, kwa sababu tayari damu yake ishakuwa haramu, kwa sababu ikiwa utamuua baada ya kusilimu kwake; basi hakika yeye atakuwa katika nafasi yako ya kulindwa damu kwa Uislamu wake, na wewe utakuwa katika nafasi yake, itakuwa halali damu yako kwa kukuua kwa kisasi kwa sababu ya kumuuwa.
Faida
- Yatakayejitokeza kwake yanayoonyesha kuingia katika Uislamu kama kauli au kitendo, ni haramu kumuua.
- Atakaposilimu mmoja kati ya makafiri wakati wa vita, basi damu yake itakingwa, na ni lazima kutomuua, isipokuwa tukibaini kinyume na hilo.
- Ni lazima muislamu matamanio yake yafuate sheria na si mihemuko na kutaka kulipiza kisasi.
- Amesema bin Hajari: Inafaa kuuliza matatizo kabla hayajatokea, kwa kuzingatia kauli sahihi kuwa kisa hiki aliuliza kabla jambo halijatokea, ama yaliyopokelewa kutoka kwa baadhi ya wema waliotangulia kulichukia hilo, hilo linatafsirika kuwa hutokea mara chache sana, ama yanayowezekana kutokea kwa kawaida ni sheria kuyaulizia ili yafahamike.
Jifanyie mazoezi
Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.