Maadili, Adabu na Tabia Njema
SOMO · Sahih Muslim · Na. 2359

Nilionyeshwa Pepo na Moto, katu sijawahi kuona katika kheri na shari mfano wa siku hiyo, na lau mngejua ninayoyajua basi mngelicheka kidogo na mngelia sana

Wema, Uadilifu na Tabia Njema

Kiarabu

عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ رضي الله عنه قَالَ: بَلَغَ رَسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم ‌عَنْ ‌أَصْحَابِهِ ‌شَيْءٌ، فَخَطَبَ فَقَالَ: «عُرِضَتْ عَلَيَّ الْجَنَّةُ وَالنَّارُ فَلَمْ أَرَ كَالْيَوْمِ فِي الْخَيْرِ وَالشَّرِّ، وَلَوْ تَعْلَمُونَ مَا أَعْلَمُ لَضَحِكْتُمْ قَلِيلًا وَلَبَكَيْتُمْ كَثِيرًا» قَالَ: فَمَا أَتَى عَلَى أَصْحَابِ رَسُولِ اللهِ صلى الله عليه وسلم يَوْمٌ أَشَدُّ مِنْهُ، قَالَ: غَطَّوْا رُءُوسَهُمْ وَلَهُمْ خَنِينٌ، قَالَ: فَقَامَ عُمَرُ فَقَالَ: رَضِينَا بِاللهِ رَبًّا، وَبِالْإِسْلَامِ دِينًا، وَبِمُحَمَّدٍ نَبِيًّا، قَالَ: فَقَامَ ذَاكَ الرَّجُلُ فَقَالَ: مَنْ أَبِي؟ قَالَ: «أَبُوكَ فُلَانٌ»، فَنَزَلَتْ: {يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لا تَسْأَلُوا عَنْ أَشْيَاءَ إِنْ تُبْدَ لَكُمْ تَسُؤْكُمْ} [المائدة: 101].

Tafsiri ya Kiswahili

Kutoka kwa Anasi bin Maliki radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Lilimfikia jambo Mtume rehema na amani ziwe juu yake kutoka kwa Maswahaba zake, akawahutubia akasema: "Nilionyeshwa Pepo na Moto, katu sijawahi kuona katika kheri na shari mfano wa siku hiyo, na lau mngejua ninayoyajua basi mngelicheka kidogo na mngelia sana" Akasema: Haikuwahi kutokea kwa Maswahaba wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake siku ngumu kama hiyo, akasema: Wakafunika nyuso zao huku wakitoa sauti za kugugumia (kwa vilio), anasema: Akasimama Omari akasema: Tumemridhia Mwenyezi Mungu kuwa Mola, na Uislamu kuwa dini, na Muhammadi kuwa Nabii, anasema: akasimama yule bwana akasema: Ni nani baba yangu? Akasema: "Baba yako ni fulani", ikateremka: "Enyi mlioamini! Msiulize mambo ambayo mkidhihirishiwa yatakuchukizeni" [Al-Maaida: 101].

English translation

Anas ibn Mālik (may Allah be pleased with him) reported: The Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) was informed about something regarding his Companions, so he delivered a sermon and said: "Paradise and Hellfire were presented to me, and I have never seen anything like today in terms of good and evil. If you knew what I know, you would laugh little and weep much." He said: The Companions of the Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) did not experience a day more difficult than that. He said: They covered their heads and made sounds of grief. He said: Then ‘Umar stood up and said: We are pleased with Allah as a Lord, with Islam as a religion, and with Muhammad as a Prophet. He said: Then that man stood up and said: Who is my father? He said: "Your father is so-and-so." Then the following verse was revealed: {O you who believe, do not ask about things that, if they were made known to you, would only cause you hardship.} [Surat al-Mā’idah: 101]

Maelezo

Lilimfikia jambo Mtume rehema na amani ziwe juu yake kutoka kwa Maswahaba zake, nalo ni kwamba wao walimzidishia maswali, akakasirika, na akawahutubia, akasema: Nimeonyeshwa Pepo na Moto; sikuwahi kuona kheri nyingi kuliko nilizoziona siku ya leo Peponi, wala shari kubwa kuliko nilizoziona siku hiyo Motoni, na lau kama mngeliona nilichokiona, na mkajua ninachokijua katika yale niliyoyaona siku ya leo na kabla ya leo, basi mngelihuzunika huzuni kubwa, na kungepungua kucheka kwenu, na kungezidi kulia kwenu. Anasema Anasi radhi za Allah ziwe juu yake: Haikuwahi kutoka kwa Maswahaba wake rehema na amani ziwe juu yake siku ngumu kama hiyo, na wakafunika vichwa vyao huku wakitoa sauti ya kunung'unika inayotoka puani kwa sababu ya kulia sana. Akasimama Omari radhi za Allah ziwe juu yake akasema: Tumemridhia Mwenyezi Mungu kuwa Mola, na Uislamu kuwa dini, na Muhammadi kuwa Nabii. Akasema: Akasimama yule bwana, akasema: Nani baba yangu? Akasema: "Baba yako ni fulani", ikateremka: "Enyi mlioamini! Msiulize kuhusu mambo ambayo yakikudhihirikieni yatakuchukizeni" [Al-Ma’idah: 101].

Faida

  • Ni Sunna kulia kwa kuhofia adhabu ya Mwenyezi Mungu, na kutokithirisha kucheka; kwa sababu hilo linaonyesha kughafilika na ugumu wa moyo.
  • Waliathirika na mawaidha Maswahaba radhi za Allah ziwe juu yao, na hofu yao kubwa dhidi ya adhabu za Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka.
  • Sunna ya kufunika uso wakati wa kulia.
  • Amesema Al-Khattwabi: Hadithi hii ni kwa mtu aliyeuliza kwa kuchokonoa mambo au kwa ukaidi katika mambo ambayo hana haja nayo, ama atakayeuliza kwa dharura, kwa kutokewa na jambo akaliulizia, huyu hana dhambi juu yake wala lawama.
  • Himizo la kuwa na msimamo katika kumtii Allah, na kujitenga mbali na kumuasi Allah, na kusimama katika mipaka ya Mwenyezi Mungu.
  • Hapa inaonyesha kufaa kukasirika wakati wa mawaidha na wakati wa kufundisha.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)