Fiqhi, Swala na Ibada
SOMO · Sahih al-Bukhari · Na. 1503

Alifaradhisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake zakatul-fitiri kibaba cha tende, au kibaba cha ngano, kwa mtumwa na aliyehuru, na mwanaume na mwanamke, na mdogo na mkubwa katika waislamu, na akaamrisha itolewe kabla ya watu kutoka kwenda katika swala

Hukumu za Swala na Tohara

Kiarabu

عَنِ ابْنِ عُمَرَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: فَرَضَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ زَكَاةَ الفِطْرِ صَاعًا مِنْ تَمْرٍ، أَوْ صَاعًا مِنْ شَعِيرٍ، عَلَى العَبْدِ وَالحُرِّ، وَالذَّكَرِ وَالأُنْثَى، وَالصَّغِيرِ وَالكَبِيرِ مِنَ المُسْلِمِينَ، وَأَمَرَ بِهَا أَنْ تُؤَدَّى قَبْلَ خُرُوجِ النَّاسِ إِلَى الصَّلاَةِ.

Tafsiri ya Kiswahili

Imepokelewa kutoka kwa bin Omari radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake, amesema: Alifaradhisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake zakatul-fitiri kibaba cha tende, au kibaba cha ngano, kwa mtumwa na aliyehuru, na mwanaume na mwanamke, na mdogo na mkubwa katika waislamu, na akaamrisha itolewe kabla ya watu kutoka kwenda katika swala.

English translation

Ibn ‘Umar (may Allah be pleased with him and his father) reported: The Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) enjoined Zakat al-Fitr as one Sā‘ of dates or one Sā‘ of barley on the slave and the free person, the male and the female, the young and the old from among the Muslims. He ordered that it be given before the people go out to the prayer.

Maelezo

Amewajibisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake zakatul-fitiri baada ya Ramadhani, nayo kwa kiwango cha kibaba inafikia uzito wake machoto manne. Na mudi moja: Ni ujazo wa viganja viwili vya mtu wa kati na kati, wa tende au ngano, kwa kila muislamu; aliye huru na mtumwa, mwanaume na mwanamke, mdogo na mkubwa, na hii ni kwa yule ambaye anachakula kinachozidi kwa siku yake hiyo na usiku wake, kwake yeye na kwa wale anaowahudumia. Na akaamrisha itolewe kabla ya watu kutoka kwenda katika swala ya Iddi.

Faida

  • Zakatul-fitiri ya Ramadhani ni lazima kutolewa kwa mtoto na mkubwa, na aliye huru na mamluki, na anasemeshwa hapa msimamizi na bosi, na anaitoa mwanaume kwa niaba yake na watoto wake na wale ambao ni wajibu kwake kuwahudumia.
  • Si wajibu zakatul-fitiri kwa kichanga kilichoko tumboni, bali inapendeza tu.
  • Kumebainishwa kinachotolewa katika zakatul-fitiri, nakuwa ni chakula cha watu walichokizoea.
  • Uwajibu wa kuitoa kabla ya swala ya Iddi, na bora zaidi iwe asubuhi ya siku ya Iddi, na inafaa kuitoa kabla ya Iddi kwa siku moja au mbili.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)