Fiqhi, Swala na Ibada
SOMO · Sahih Muslim · Na. 1082

Msiitangulizie Ramadhani kwa swaumu ya siku moja wala siku mbili, isipokuwa mtu aliyekuwa akifunga swaumu fulani basi na aifunge

Hukumu za Swala na Tohara

Kiarabu

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «لَا تَقَدَّمُوا رَمَضَانَ بِصَوْمِ يَوْمٍ وَلَا يَوْمَيْنِ إِلَّا رَجُلٌ كَانَ يَصُومُ صَوْمًا فَلْيَصُمْهُ».

Tafsiri ya Kiswahili

Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Msiitangulizie Ramadhani kwa swaumu ya siku moja wala siku mbili, isipokuwa mtu aliyekuwa akifunga swaumu fulani basi na aifunge".

English translation

Abu Hurayrah (may Allah be pleased with him) reported: The Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "Do not precede Ramadan by fasting a day or two unless a man has a habitual fast, then let him fast it."

Maelezo

Amemkataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake muislamu kufunga kabla ya Ramadhani kwa siku moja au siku mbili, kwa nia ya kuchukua tahadhari kuwa huenda Ramadhani imeingia; kwa sababu ulazima wa Ramadhani umewekwa katika kuonekana kwa mwandamo, na wala hakuna haja ya kujikalifisha, isipokuwa kama mtu alikuwa akifunga swaumu aliyoizoea, kama kufunga siku moja na kula siku moja, au siku ya juma tatu na Alhamisi ikaangukia siku hiyo basi na afunge; na wala hilo halihesabiki kuwa ni katika kuipokea Ramadhani, na inaunganishwa hapo swaumu zitakazokuwa za wajibu kama kulipa deni na swaumu ya nadhiri.

Faida

  • Katazo la kujilazimisha, na uwajibu wa kuzihifadhi ibada kama zilivyowekwa na sheria pasina kuzidisha au kupunguza.
  • Miongoni mwa hekima za hilo -na Allah ndiye mjuzi zaidi- ni kutofautisha kati ya ibada za faradhi na sunna, na kujiandaa kwa Ramadhani kwa uchangamfu na shauku, na ili swaumu iwe ndiyo nembo ya mwezi mtukufu yenye kujipambanua nayo.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)