Maadili, Adabu na Tabia Njema
SOMO · Sahih Muslim · Na. 213

Hakika mtu mwenye adhabu nafuu katika watu wa motoni ni yule atakayekuwa na viatu viwili na soli mbili vitokanavyo na moto, utakuwa ukitokota kwa hivyo ubongo wake kama kinavyotokota chungu, hatoona kuwa kuna yeyote mwenye adhabu kali kuliko yeye, kumbe yeye ndiye ana adhabu nafuu kuliko wote

Wema, Uadilifu na Tabia Njema

Kiarabu

عَنِ النُّعْمَانِ بْنِ بَشِيرٍ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «إِنَّ أَهْوَنَ أَهْلِ النَّارِ عَذَابًا مَنْ لَهُ نَعْلَانِ وَشِرَاكَانِ مِنْ نَارٍ، يَغْلِي مِنْهُمَا دِمَاغُهُ كَمَا يَغْلِ الْمِرْجَلُ، مَا يَرَى أَنَّ أَحَدًا أَشَدُّ مِنْهُ عَذَابًا، وَإِنَّهُ لَأَهْوَنُهُمْ عَذَابًا».

Tafsiri ya Kiswahili

kutoka kwa Nu'man bin Bashiri -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake-: "Hakika mtu mwenye adhabu nafuu katika watu wa motoni ni yule atakayekuwa na viatu viwili na soli mbili vitokanavyo na moto, utakuwa ukitokota kwa hivyo ubongo wake kama kinavyotokota chungu, hatoona kuwa kuna yeyote mwenye adhabu kali kuliko yeye, kumbe yeye ndiye ana adhabu nafuu kuliko wote"

English translation

An-Nu‘mān ibn Bashīr (may Allah be pleased with him) reported: The Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "The least tortured among the dwellers of Hellfire is a person who has two shoes and two shoelaces made of fire that will cause his brain to boil as a boiling cauldron. He thinks that none is more severely tortured than him, although he is the least tortured among them."

Maelezo

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa mtu mwenye adhabu nafuu katika watu wa motoni siku ya Kiyama ni yule atayekuwa na viatu viwili na soli mbili, utakuwa ukichemka ubongo wake kutokana na kuchemka kwake, kama linavyochemka sufuria la shaba, na wala hatoona kuwa kuna yeyote mwenye adhabu kali zaidi yake, kumbe yeye ndiye mwenye adhabu nafuu zaidi kuliko wote, na hii ni kwa sababu zitakusanyika kwake adhabu zote mbili, adhabu ya mwili na adhabu ya nafsi.

Faida

  • Tahadhari hii ni kwa wanaoasi na makafiri kutokana na vitisho vya adhabu hii motoni; ili wajitenge mbali na yale yanayopelekea huko.
  • Kutofautiana kwa vina vya waoingia motoni kulingana na ubaya wa matendp yao.
  • Ukali wa adhabu ya moto, tunamuomba Allah atusalimishenayo.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)