Muislamu atakapoulizwa kaburini anashuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, nakuwa Muhammadi ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu
Tawhid na Kumtii Mwenyezi Mungu
Kiarabu
عَنِ البَرَاءِ بْنِ عَازِبٍ رضي الله عنه أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «المُسْلِمُ إِذَا سُئِلَ فِي القَبْرِ: يَشْهَدُ أَنْ لاَ إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ وَأَنَّ مُحَمَّدًا رَسُولُ اللَّهِ»، فَذَلِكَ قَوْلُهُ: {يُثَبِّتُ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا بِالقَوْلِ الثَّابِتِ فِي الحَيَاةِ الدُّنْيَا وَفِي الآخِرَةِ} [إبراهيم: 27].
Tafsiri ya Kiswahili
kutoka kwa Albaraa bin Aazib Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema: "Muislamu atakapoulizwa kaburini anashuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, nakuwa Muhammadi ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu", Hiyo ndiyo kauli yake Mtukufu: "Huwapa umakinifu Mwenyezi Mungu wale walioamani kwa kauli thabiti katika maisha ya dunia na katika akhera" [Ibrahim: 27].
English translation
Al-Barā’ ibn ‘Āzib (may Allah be pleased with him) reported that the Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "When a Muslim is questioned in the grave, he testifies that no deity is worthy of worship except Allah and that Muhammad is the Messenger of Allah," this is His saying: {Allah keeps those who believe steadfast with the firm Word [of faith] in the life of this world and in the Hereafter.} [Surat Ibrāhīm: 27]
Maelezo
Muumini ataulizwa kaburini, watamuuliza Malaika wawili waliopangiwa kufanya hivyo, nao ni Munkari na Nakiri, kama walivyotajwa katika Hadithi kadhaa, atashuhudia kuwa hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu na kuwa Muhammadi ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, Akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake, hii ndio kauli thabiti aliyoisema Mwenyezi Mungu: "Huwapa umakinifu Mwenyezi Mungu wale walioamani kwa kauli thabiti katika maisha ya dunia na katika akhera" [Surat Ibrahim: 27].
Faida
- Nikuwa maswali ya kaburini ni kweli yapo.
- Fadhila ya Mwenyezi Mungu Mtukufu juu ya waja wake waumini katika dunia na akahera anawapa nguvu kwa kauli thabiti.
- Ubora wa shahada ya tauhidi na kufa juu yake.
- Mwenyezi Mungu kumpa thabati (nguvu) Muumini katika dunia ni kwa kumpa msimamo katika imani, na kutembea katika njia iliyonyooka, na wakati wa kufa kwa kufa katika tauhidi, na kaburini wakati akiulizwa na Malaika wawili.
Jifanyie mazoezi
Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.