Fiqhi, Swala na Ibada
SOMO · Sahih al-Bukhari · Na. 3270

Alitajwa kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake mtu mmoja aliyelala usiku mpaka pakapambazuka, akasema: "Huyo ni mtu aliyekojolewa na Shetani ndani ya masikio yake, au alisema: ndani ya sikio lake

Hukumu za Swala na Tohara

Kiarabu

عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بنِ مسعُودٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: ذُكِرَ عِنْدَ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ رَجُلٌ نَامَ لَيْلَهُ حَتَّى أَصْبَحَ، قَالَ: «ذَاكَ رَجُلٌ بَالَ الشَّيْطَانُ فِي أُذُنَيْهِ، أَوْ قَالَ: فِي أُذُنِهِ».

Tafsiri ya Kiswahili

Imepokelewa kutoka kwa Abdullahi bin Masoud -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Alitajwa kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake mtu mmoja aliyelala usiku mpaka pakapambazuka, akasema: "Huyo ni mtu aliyekojolewa na Shetani ndani ya masikio yake, au alisema: ndani ya sikio lake".

English translation

‘Abdullah ibn Mas‘ūd (may Allah be pleased with him) reported: It was mentioned before the Prophet (may Allah's peace and blessings be upon him) about a man who slept throughout the night until morning. He said, "That is a man in whose ears—or, he said, in whose ear—the devil urinated."

Maelezo

Alitajwa kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake mtu mmoja aliyelala mpaka pakapambazuka na Jua likachomoza na wala hakunyanyuka kwenda katika swala ya faradhi, akasema rehema na amani ziwe juu yake: Huyo ni mtu ambaye Shetani kakojoa ndani ya sikio lake.

Faida

  • Ni karaha kuacha kusimama usiku, nakuwa hilo ni kwa sababu ya Shetani.
  • Kutahadhari na Shetani anayemkalia mwanadam katika njia zote; ili amkinge na kuzuia kati yake na kumtii Mwenyezi Mungu Mtukufu.
  • Amesema bin Hajari: Kauli yake: "Hakusimama kuswali" Makusudio yake ni aina ya sala, na inawezekana kuwa ni ahadi, na inakusudiwa ni swala ya usiku au swala ya faradhi.
  • Amesema Twaibi: Limetajwa sikio pekee, japokuwa jicho ndio linastahiki zaidi kulala ikiwa ni ishara ya uzito wa usingizi, kwa sababu masikio ndio nyenzo za umakini, na umetajwa mkojo; kwa sababu ndio mwepesi kupenya katika njia za sikio, na mwepesi kutembea katika mishipa, na kusababisha uvivu katika viungo vyote.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)