Aqidah na Misingi ya Imani
SOMO · Sahih Muslim · Na. 2674

Atakayelingania katika uongofu, atakuwa kwake kapata malipo mfano wa malipo ya aliyemfuata, halipunguzi hilo chochote katika malipo yao

Tawhid na Kumtii Mwenyezi Mungu

Kiarabu

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه أَنَّ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «مَنْ دَعَا إِلَى هُدًى كَانَ لَهُ مِنَ الْأَجْرِ مِثْلُ أُجُورِ مَنْ تَبِعَهُ، لَا يَنْقُصُ ذَلِكَ مِنْ أُجُورِهِمْ شَيْئًا، وَمَنْ دَعَا إِلَى ضَلَالَةٍ كَانَ عَلَيْهِ مِنَ الْإِثْمِ مِثْلُ آثَامِ مَنْ تَبِعَهُ، لَا يَنْقُصُ ذَلِكَ مِنْ آثَامِهِمْ شَيْئًا».

Tafsiri ya Kiswahili

Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakayelingania katika uongofu, atakuwa kwake kapata malipo mfano wa malipo ya aliyemfuata, halipunguzi hilo chochote katika malipo yao, na atakayelingania katika upotofu atakuwa kwake na madhambi mfano wa madhambi ya yule aliyemfuata, halipunguzi hilo katika madhambi yao chochote".

English translation

Abu Hurayrah (may Allah be pleased with him) reported that the Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "Whoever calls to guidance shall receive a reward similar to the rewards obtained by those who followed him without diminishing anything from their rewards. And whoever calls to misguidance shall incur a sin similar to the sins incurred by those who followed him without diminishing anything from their sins."

Maelezo

Amebainisha Mtume Rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakayewaelekeza na kuwajulisha na kuwahamasisha watu katika njia ya haki na kheri kwa kauli au kitendo, basi atakuwa na malipo mfano wa malipo atakayoyapata aliyemfuata katika hilo, na hilo halitopunguza katika malipo ya mfanyaji chochote. Na atakaye waelekeza watu na kuwaonyesha njia ya batili na shari ambayo ina dhambi ndani yake na makosa au jambo lisilo la halali, kwa kauli au kitendo, basi atakuwa na madhambi mfano wa madhambi ya yule atakayemfuata, pasina ya kupunguza hilo katika madhambi yao chochote.

Faida

  • Fadhila za kuwaita watu katika uongofu, uwe mdogo au mkubwa, na kuwa mwenye kuwaita watu katika uongofu ana malipo mfano wa malipo ya mfanyaji, na hilo ni katika fadhila kubwa za Allah na ukarimu wake uliokamilika.
  • Hatari ya kuhamasisha upotofu, uwe kidogo au mwingi, nakuwa mwenye kuhimiza katika upotofu ana madhambi mfano wa mfanyaji.
  • Malipo huendana na matendo, atakayelingania katika kheri atapata malipo mfano wa mfanyaji wake, na atakayelingania katika shari atapata mfano wa madhambi ya mfanyaji wake.
  • Ni juu ya muislamu atahadhari kwa wale wenye kumuiga kwa kudhihirisha kwake maasi na watu wakimuona, kwani anapata dhambi kupitia atakayemuiga hata kama hajamhamasisha juu ya hilo.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)