Maadili, Adabu na Tabia Njema
SOMO · Sahih al-Bukhari · Na. 2896

Hakuna msaada na riziki mnayopewa nyinyi isipokuwa ni kupitia kwa watu madhaifu wenu

Wema, Uadilifu na Tabia Njema

Kiarabu

عَنْ مُصْعَبِ بْنِ سَعْدٍ قَالَ: رَأَى سَعْدٌ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ أَنَّ لَهُ فَضْلًا عَلَى مَنْ دُونَهُ، فَقَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «هَلْ تُنْصَرُونَ وَتُرْزَقُونَ إِلَّا بِضُعَفَائِكُمْ».

Tafsiri ya Kiswahili

Kutoka kwa Mus'abu bin Saadi amesema: Alijiona Saadi radhi za Allah ziwe juu yake kuwa yeye ana thamani kuliko aliye chini yake, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Hakuna msaada na riziki mnayopewa nyinyi isipokuwa ni kupitia kwa watu madhaifu wenu".

English translation

Mus‘ab ibn Sa‘d reported: Sa‘d (may Allah be pleased with him) saw that he had superiority over those beneath him. So, the Prophet (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "Are you granted victory and provided with sustenance except through your weak ones?"

Maelezo

Alidhania Saadi bin Abii Waqas radhi za Allah ziwe juu yake kuwa yeye ana ubora kuliko aliye chini yake katika watu madhaifu, kwa sababu ya ushujaa wake na mfano wa hilo!. Akasema rehema na amani ziwe juu yake: Tambueni kuwa hamnusuriwi wala hampewi riziki isipokuwa kwa watu wenu madhaifu kwa dua zao na swala zao na utakasifu wao wa nia; kwani wao mara nyingi ndio hutakasa dua zaidi, na huwa na unyenyekevu zaidi katika ibada kwa sababu nyoyo zao ziko tupu hazifungamani na mapambo ya dunia.

Faida

  • Himizo la kuwa mnyenyekevu na katazo la kujiona bora kwa watu wengine.
  • Amesema bin Hajari: Ikiwa mwenye nguvu anakuwa na hadhi kwa ubora wa ushujaa wake, basi mtu dhaifu anakuwa bora kwa dua yake na utakasifu wa nia yake (Ikhlas yake).
  • Himizo la kutenda wema kwa mafakiri na kuwapa haki zao, kwani hilo ni katika sababu za kupata rehema ya Mwenyezi Mungu kwako na msaada wake.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)