Fiqhi, Swala na Ibada
SOMO · Sahih al-Bukhari · Na. 272

Alikuwa Mtume Rehema na amani ziwe juu yake anapooga kwa ajili ya janaba, anaosha mikono yake, na anatawadha udhu wake ule wa swala, kisha anaoga

Hukumu za Swala na Tohara

Kiarabu

عَنْ عَائِشَةَ أُمِّ المؤمنين رضي الله عنها قَالَتْ: كَانَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِذَا اغْتَسَلَ مِنَ الجَنَابَةِ، غَسَلَ يَدَيْهِ، وَتَوَضَّأَ وُضُوءَهُ لِلصَّلاَةِ، ثُمَّ اغْتَسَلَ، ثُمَّ يُخَلِّلُ بِيَدِهِ شَعَرَهُ، حَتَّى إِذَا ظَنَّ أَنَّهُ قَدْ أَرْوَى بَشَرَتَهُ، أَفَاضَ عَلَيْهِ المَاءَ ثَلاَثَ مَرَّاتٍ، ثُمَّ غَسَلَ سَائِرَ جَسَدِهِ، وَقَالَتْ: كُنْتُ أَغْتَسِلُ أَنَا وَرَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مِنْ إِنَاءٍ وَاحِدٍ، نَغْرِفُ مِنْهُ جَمِيعًا.

Tafsiri ya Kiswahili

Imepokewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini Radhi za Allah ziwe juu yake: Alikuwa Mtume Rehema na amani ziwe juu yake anapooga kwa ajili ya janaba, anaosha mikono yake, na anatawadha udhu wake ule wa swala, kisha anaoga, kisha anaachanisha nywele zake kwa mkono wake, mpaka pale anapohisi kuwa ngozi yake yote imeenea maji, anajimwagia maji kwa michoto mitatu, kisha anaosha mwili wake wote uliobakia, na Aisha akasema: Nilikuwa nikioga mimi na Mtume Rehema na amani ziwe juu yake katika chombo kimoja, tukichota sote katika chombo hicho.

English translation

‘Ā’ishah, the Mother of the Believers, (may Allah be pleased with her) reported: On taking a ritual bath from Janābah (major ritual impurity), the Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) used to wash his hands and perform ablution like that for prayer, then wash himself. He would, then, run his wet hand through his hair until he would feel that his skin had become wet. Then, he would pour water thrice over it, and then wash the rest of his body. She further said: I and the Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) used to bathe from a single container from which we used to take water simultaneously.

Maelezo

Alikuwa Mtume Rehema na amani ziwe juu yake anapotaka kuoga janaba anaanza kwa kuosha mikono yake, kisha anatawadha kama anavyotawadha udhu wa swala, kisha anajimwagia maji katika mwili wake kisha anaachanisha nywele za kichwa chake kwa mikono yake, mpaka anapohisi kuwa maji yamefika katika maoteo ya nywele zake, na yameloanisha ngozi, anajimwagia maji kichwani mara tatu kisha anaosha mwili mzima. Na akasema Aisha Radhi za Allah ziwe juu yake: Nilikuwa nikioga mimi pamoja na Mtume Rehema na amani ziwe juu yake kutoka katika chombo kimoja, tukichota sote.

Faida

  • Josho lina aina mbili: Linalotosheleza na lilokuwa kamili, ama josho linalotosheleza ni mtu kunuia twahara, kisha akaeneza maji katika mwili wake ikiwa ni pamoja na kupandisha maji puani na kusukutua, na ama josho lilokuwa kuwa kamili ataoga kama alivyo oga Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika hadithi hii.
  • Neno Janaba hutumika kwa kila aliyetoa manii, au kafanya tendo la ndoa hata kama hajamtoka.
  • Inaruhusiwa mwanandoa kutazama uchi wa mwenzake, na kuoga pamoja katika chombo kimoja.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)