Maadili, Adabu na Tabia Njema
SOMO · Sahih al-Bukhari · Na. 3282

Hakika mimi ninajua neno ambalo lau kama angelisema yangemuondokea anayaoyapata (katika hasira), lau angesema: Audhubillaahi minash-shaitwani, -Najilinda kwa Mwenyezi Mungu kutokana na Shetani- ingemuondokea hasira anayoipata

Wema, Uadilifu na Tabia Njema

Kiarabu

عَنْ سُلَيْمَانَ بْنِ صُرَدٍ رضي الله عنه قَالَ: كُنْتُ جَالِسًا مَعَ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَرَجُلاَنِ يَسْتَبَّانِ، فَأَحَدُهُمَا احْمَرَّ وَجْهُهُ، وَانْتَفَخَتْ أَوْدَاجُهُ، فَقَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «إِنِّي لَأَعْلَمُ كَلِمَةً لَوْ قَالَهَا ذَهَبَ عَنْهُ مَا يَجِدُ، لَوْ قَالَ: أَعُوذُ بِاللَّهِ مِنَ الشَّيْطَانِ، ذَهَبَ عَنْهُ مَا يَجِدُ» فَقَالُوا لَهُ: إِنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «تَعَوَّذْ بِاللَّهِ مِنَ الشَّيْطَانِ»، فَقَالَ: وَهَلْ بِي جُنُونٌ؟

Tafsiri ya Kiswahili

Kutoka kwa Salmaani bin Swurad -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilikuwa nimekaa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake na kukawa na watu wawili wakitukanana, mmoja wao uso wake ulikuwa mwekundu (kwa hasira) na ikavimba mishipa yake ya shingo, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Hakika mimi ninajua neno ambalo lau kama angelisema yangemuondokea anayaoyapata (katika hasira), lau angesema: Audhubillaahi minash-shaitwani, -Najilinda kwa Mwenyezi Mungu kutokana na Shetani- ingemuondokea hasira anayoipata" Wakasema kumwambia: Hakika Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: Jikinge kwa Mwenyezi Mungu kutokana na Shetani", akasema: Hivi mimi ninawendawazimu?

English translation

Sulaymān ibn Surad (may Allah be pleased with him) reported: I was sitting with the Prophet (may Allah's peace and blessings be upon him) when two men started to insult each other, and the face of one of them turned red and his jugular veins got swollen. The Prophet (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "Verily, I know a word; if he said it, his rage would go away. If he said: I seek refuge with Allah from the devil, his rage would go away." They said to him: The Prophet (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "Seek refuge with Allah from the devil." Thereupon he said: Am I mad?

Maelezo

Walitukanana na kushutumiana watu wawili mbele ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na ukawa mwekundu uso wa mmoja wao na ikavimba mishipa inayozunguka shingo yake. Akasema rehema na amani ziwe juu yake: Hakika mimi ninajua neno ambalo lau angelisema huyu aliyekasirika basi hasira zingemuondokea, lau angesema: Audhubillaahi mina sh-shaitwanir rajiim - Najilinda kwa Mwenyezi Mungu kutokana na Shetani aliyelaaniwa. Wakasema kumwambia: Hakika Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: Jilinde kwa Mwenyezi Mungu kutokana na Shetani. Akasema: Hivi mimi ni mwendawazimu?! Alidhania kuwa hajilindi na Shetani isipokuwa mwenye wazimu.

Faida

  • Pupa ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika kutoa muongozo na kuelekeza, panapopatikana sababu zake.
  • Hasira hutokana na Shetani.
  • Amri ya kujilinda kwa Mwenyezi Mungu kutokana na Shetani aliyelaaniwa wakati wa hasira, amesema Mtukufu: "Na ikiwa uchochezi wa Shetani utakuchochea basi omba ulinzi wa Mwenyezi Mungu.." Mpaka mwisho wa Aya.
  • Tahadhari ya kutoa matusi na yenye kufanana na matusi kama kutoa laana, na chukizo la hayo; kwa sababu mambo haya hupelekea katika uharibifu baina ya watu.
  • Kunukuu nasaha kumpelekea ambaye hajazisikia ili anufaike nazo.
  • Ametahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake dhidi ya hasira; kwa sababu husukuma katika shari na ugomvi, na alikuwa rehema na amani ziwe juu yake hakasiriki isipokuwa yanapotendwa maharamisho ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na hii ndio hasira nzuri.
  • Amesema Imam Nawawi katika kauli yake "Kwani unaniona mimi ninawazimu": Kauli hii inaonyesha kuwa msemaji alikuwa ni miongoni mwa wanafiki, au ni katika mabedui wakorofi.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)