Maadili, Adabu na Tabia Njema
SOMO · Sahih Muslim · Na. 2021

Amesimulia kuwa mtu mmoja alikula chakula kwa Mtume Rehema na amani ziwe juu yake kwa mkono wake wa kushoto, akasema: "Kula kwa mkono wako wa kulia", Akasema: Siwezi, akasema: "Kamwe, hutoweza!",

Wema, Uadilifu na Tabia Njema

Kiarabu

عَنْ سَلَمَةَ بْنِ الْأَكْوَعِ رضي الله عنه: أَنَّ رَجُلًا أَكَلَ عِنْدَ رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِشِمَالِهِ، فَقَالَ: «كُلْ بِيَمِينِكَ»، قَالَ: لَا أَسْتَطِيعُ، قَالَ: «لَا اسْتَطَعْتَ»، مَا مَنَعَهُ إِلَّا الْكِبْرُ، قَالَ: فَمَا رَفَعَهَا إِلَى فِيهِ.

Tafsiri ya Kiswahili

Kutoka kwa Salama bin Al Ak'wa'i -Radhi za Allah ziwe juu yake. Amesimulia kuwa mtu mmoja alikula chakula kwa Mtume Rehema na amani ziwe juu yake kwa mkono wake wa kushoto, akasema: "Kula kwa mkono wako wa kulia", Akasema: Siwezi, akasema: "Kamwe, hutoweza!", Hakuna kilichomzuia ila ni kiburi, akasema: hakuweza tena kuunyanyua kwenda kinywani kwake.

English translation

Salamah ibn al-Akwa‘ (may Allah be pleased with him) reported: A man ate with his left hand in the presence of the Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him), whereupon he said: "Eat with your right hand." The man said: I cannot do that. Thereupon, he said: "May you not be able to do that." It was only arrogance that prevented him. He said: He could not raise it up to his mouth afterward.

Maelezo

Alimuona Mtume Rehema na amani ziwe juu yake mtu mmoja akila kwa mkono wake wa kushoto, akamuamrisha ale kwa mkono wake wa kulia, Yule bwana akamjibu kwa kiburi na kwa kuongopa kuwa hawezi! Mtume Rehema na amani ziwe juu yake akamuombea dua mbaya azuiliwe kula kwa mkono wa kulia, Mwenyezi Mungu akajibu dua ya Nabii wake, kwa kupooza mkono wake wa kulia, hakuweza kuunyanyua kwenda kinywani kwake baada ya hapo kwa chakula au kinywaji.

Faida

  • Uwajibu wa kula kwa mkono wa kulia, na uharamu wa kula kwa mkono wa kushoto.
  • Kiburi katika kutekeleza hukumu za sheria mwenye kufanya hivyo anastahiki adhabu.
  • Ukarimu wa Mwenyezi Mungu kwa Nabii wake Muhammadi Rehema na amani ziwe juu yake kwa kujibu maombi yake.
  • Sheria ya kuamrisha mema na kukataza maovu kwa kila hali hata wakati wa chakula.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)